Manchester City yatwaa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Manchester United kwa penati

Manchester City yatwaa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Manchester United kwa penati

Mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Wembley iliashiria ufunguzi mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Kikosi cha Manchester City kikifurahia ushindi wao wa Ngao ya Jamii dhid ya watani wao wa jadi, Manchester United./Picha: Getty

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) Manchester City wamewafunga Manchester United mabao 7-6 kwa njia ya penati na kushinda taji la Ngao ya Jamii, siku ya Jumamosi, Agosti 10, 2024.

Hapo awali, mchezo huo ambao huashiria ufunguzi mpya wa pazia la Ligi Kuu ya Uingereza, ulimalizika kwa sare pacha ya 1-1, hatua iliyowalazimu kwenda kwenye changamoto za penati.

Manchester United, ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la FA, ndio waliotengeneza nafasi nyingi na jitihada zao zikizaa matunda katika dakika 82 ya mchezo, kupitia kwa Alejandro Garnacho.

Ilionekana wazi kuwa vijana wa Erik ten Hag wangeshinda pambano hilo hata hivyo kiungo Bernardo Silva wa Manchester City alikuwa na mawazo mengine akilini mwake, baada kuzawazisha katika dakika za lala salama, na kulazimu mikwaju ya penati ipigwe ili bingwa apatikane.

TRT Afrika