Cole Palmer asherehekea kwa kuipa Chelsea bao la kusawazisha kwenye mechi ya kusisimua ya 4-4 dhidi ya klabu yake ya zamani Manchester City Jumapili. / Picha: Reuters

Katika mojawapo ya mechi bora za msimu, Palmer aliwahi mkwaju wake hadi golini na kuwavunja City moyo baada ya viongozi hao kuchukua uongozi mara tatu ugani Stamford Bridge, Jumapili.

Palmer alifanya uhamisho wa kushangaza wa pauni milioni 42 (£milioni 51) hadi Chelsea mwezi Septemba na mechi yake wa kwanza dhidi ya mabingwa wa Ligi kuu Man City umeacha kumbukumbu.

Ilikuwa ni mchuano wenye hisia kwa mzaliwa wa Manchester Palmer, ambaye alimaliza miaka 15 katika mji huo baada ya kujiunga nao akiwa na umri wa miaka sita.

Palmer aliibuka kama mmoja wa vipaji wa vijana wa City kabla ya kuchukua uamuzi wa kujiunga na Chelsea kutafuta muda zaidi wa kucheza mara kwa mara.

Alipoulizwa iwapo aliwaudhi marafiki huko Manchester, chipukizi huyo wa miaka 21 alisema: "Ndio, labda. Najua mashabiki wengi wa City. Lakini hiyo ndio kawaida wa mchezo, sivyo?

"Ni ajabu sana, mara ya kwanza nimecheza dhidi ya City tangu niondoke, lakini nina heshima kubwa kwa klabu ambayo nilitumikia miaka 15.

"Ilikuwa nzuri kuona marafiki wengine. Kwa bahati mbaya si kupata ushindi, lakini ilikuwa mchezo mwingine mkubwa.

"Ilikuwa muda mrefu kusubiri (penalti) lakini nilihisi kujiamini. Nimekuwa na mikwaju chache.

"Nilikua tu mtulivu, niliendelea kuzingatia. Sifanyi mazoezi ya panelti, lakini ninaamini uwezo wangu wa asili na kwa shukrani iliingia," alisema.

AFP