Mikel Arteta aliita ushindi wa Newcastle wa 1-0 dhidi ya Arsenal "dhulma" baada ya bao la ushindi la Anthony Gordon kuruhusiwa kusimama na VAR. / Picha: Reuters

Klabu ya Soka ya Uingereza, Arsenal imetoa taarifa ikisema, "inaunga mkono vikamilifu maoni ya kocha Mikel Arteta baada ya Mechi dhidi ya Newcastle kufuatia uamuzi usiokubalika na makosa ya VAR jumamosi jioni."

"Matokeo haya hayapaswi kuwa yalivyo. Aibu kilichotokea, jinsi goli hili linapokubaliwa, kwenye Ligi Kuu, ligi tunayosema ni bora duniani, " Arteta alisema.

"Nimekuwa katika nchi hii kwa miaka 20 na sasa ninaona aibu. Ni aibu na kuna mengi hatarini hapa."

Arsenal imeachwa pointi tatu nyuma ya viongozi wa ligi Manchester City, baada ya kufungwa 1-0 na Newcastle, matokeo ambayo yanaweza kuwa na athari kubwa kwa matumaini yao ya taji msimu huu.

Lakini Arsenal walighadhabishwa na bao hilo, wakidai lilipaswa kukataliwa kwa kosa la ikabu (rafu) la Joelinton dhidi ya beki Gabriel.

Joelinton alionekana kumsukuma mlinzi wa Arsenal Gabriel nyuma wakati wawili hao waliwania krosi ya Joe Willock, na mpira ukimsongea Gordon aliyeelekeza wavuni kutoka eneo lililokaribia mstari wa lango.

Tetesi za ubaguzi wa rangi

Baada ya ukaguzi wa muda mrefu wa VAR, iliamuliwa hakukuwa na kosa, wakati rufaa ya Arsenal kwamba mpira uliondoka nje ya mchezo kabla ya Willock kuvuka pia ilipuuzwa, ikiwa pamoja na madai kwamba Gordon alikuwa ameuotea mpira.

"Tunaunga mkono juhudi zinazoendelea za Afisa mkuu wa waamuzi, Howard Webb na tunakaribisha ushirikiano wa pamoja ili kufikia viwango vya uamuzi vya kiwango cha ulimwengu, kulingana na mahitaji yetu ya ligi.

Newcastle iliichapa Arsenal 1-0 Jumamosi kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). / Picha: Reuters

Newcastle inakabiliana na ubaguzi wa rangi

Newcastle United wamelaani unyanyasaji wa kibaguzi uliotumwa kwa Bruno Guimaraes na Joe Willock kwenye mitandao ya kijamii kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal Jumamosi kwenye Ligi ya Premia.

"Ujumbe wetu uko wazi. Hakuna nafasi ya ubaguzi wa rangi katika soka au jamii," klabu hiyo ilisema.

"Tunatoa msaada kwa Bruno na Joe na tutashirikiana na mamlaka husika na mitandao ya kijamii kubaini waliohusika ili waweze kuwajibika."

Kichapo hicho cha pili dhidi ya Arsenal wiki hii ilikuwa pigo kubwa kwa safari yao ya taji msimu huu, ikishuhudia siku chache za matokeo mabaya baada ya pia kutemwa nje ya Kombe la ligi na West ham jumatano.

TRT Afrika