UEFA imesema inamchunguza nyota wa Uingereza Jude Bellingham kwa "ukiukaji unaowezekana wa kanuni za msingi za maadili mema" juu ya ishara aliyoifanya baada ya kufunga bao lake la kusawazisha dhidi ya Slovakia siku ya Jumapili.
"Mkaguzi wa Maadili na Nidhamu wa UEFA atafanya uchunguzi wa kinidhamu kuhusiana na uwezekano wa ukiukaji wa kanuni za msingi za maadili ya mchezaji wa Shirikisho la Soka la Uingereza, Jude Bellingham, kutokana na kudaiwa kutokea katika uwanja wa mechi hii," bodi inayosimamia soka barani Ulaya ilisema. katika taarifa ya Jumatatu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alifunga bao la kusawazisha dakika za majeruhi dhidi ya Slovakia katika mechi ya EURO 2024 hatua ya 16 bora, ambayo England ilishinda 2-1.
Kiungo huyo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Uingereza alifunga mkwaju wa juu katika dakika ya 95 na kuifanya England kuendelea kubaki katika mchezo huo, na baada ya bao lake la hali ya juu Bellingham alionekana akifanya ishara ya kushika sehemu ya uume wake akielekeza ishara kwa benchi ya Slovakia.
Hata hivyo, Bellingham alijieleza katika mtandao wa X kuwa ihsara hiyo haikuelekezewa wachezaji wa Slovakia.
''Ishara ya utani ya ndani kwa baadhi ya marafiki wa karibu waliokuwa kwenye mchezo. Hakuna ila heshima kwa jinsi timu hiyo ya Slovakia ilivyocheza usiku wa leo,'' alisema Bellingham.