Nuksi za Penalti zawavunjwa moyo tena Malkia wa Nigeria kwenye Kombe la Dunia la Wanawake

Nuksi za Penalti zawavunjwa moyo tena Malkia wa Nigeria kwenye Kombe la Dunia la Wanawake

Falcons iliweka hitoria kwa kuwa timu ya kwanza ya Kiafrika kutofungwa katika mechi za hatua ya makundi ya Kombe la Dunia.
Nigeria imepoteza 4-2 dhidi ya Uingereza kupitia mikwaju ya penalti.  / Picha: Reuters

Hatimaye safari ya Nigeria kwenye kombe la dunia la wanawake linaloendelea Australia na New Zealanda imefika kikomo baada ya 'Super Falcons' kufungwa kupitia njia ya penalti na Uingereza kwenye mechi ya kuvutia iliyochezwa dakika 120.

Rachel Daly, Alex Greenwood, Chloe Kelly, na Beth England walitia kimiani penalti za Uingereza na kujihakikishia tiketi ya robo fainali, licha ya kupoteza mkwaju wake wa kwanza uliopigwa na Georgia Stanway.

Nguvu mpya Desire Oparanozie wa Nigeria alichelea kutumia fursa ya kupachika wavuni penalti ya kwanza ya falcons baada ya Georgia Stanway kupangua penalti ya kwanza ya Uingereza. Masaibu ya Nigeria yalizidi baada ya Michelle Alozie naye kutoa nje penalti yake.

Ingawa Rasheedat Ajibade, na Christy Ucheibe waliifungia Nigeria, hayakutosha kufufua matumaini ya mabinti hao waliokuwa wakipigiwa upatu baada ya safari yao ya kuvutia ya Kombe la Dunia.

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu ni miongoni mwa wengi waliotuma jumbe za kuwamotisha mabinti hao baada ya matokeo hayo ya kuvunja moyo

"Lazima nipongeze juhudi za 'Super Falcons' kwenye Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake. Utendaji wenu mzuri haupiti bila kutambuliwa licha ya matokeo ya mwisho. Umeifanya Nigeria kujivunia kwenye jukwaa la kimataifa!" Aliandika.

Hii si mara ya kwanza timu ya kina dada ya Nigeria kutemwa nje ya hatua ya mchujo kupitia njia ya penalti, kwani mwaka uliopita, walipoteza 4-5 kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Morocco kwenye nusu fainali ya Kombe la Mataifa bora Afrika kwa Wanawake.

Hata hivyo safari ya Nigeria imewavutia sifa malkia hao kwani wamemaliza mechi za hatua ya makundi bila ya kupoteza mechi na kutoka sare na Uingerea ambao ndio mabingwa wa bara Uropa na viongozi wa Kundi D.

Uingereza sasa imetua robo fainalia na kujiunga na Uhispania, Uholanzi, Japan, na Sweden huku ikisubiri kukwatuana na mshindi wa mechi kati ya Colombia na Jamaica siku ya Jumamosi.

Lauren James alipokea kadi nyekundu kwa kufanya vurugu, akimkanyaga Alozie | Picha: Twitter ESPN

Baada ya Nigeria kuandamana na Afrika Kusini nje ya ngarambe hizo za kufana, Matumaini ya Afrika sasa yamesalia kwa timu ya Morocco maarufu 'Atlas Lionesses' itakayoshuka dimbani siku ya Jumanne kumenyana na Ufaranasa.

TRT Afrika