Kylian Mbappe alifunga mara mbili wakati Paris Saint-Germain ikibadilisha kipigo chake cha mkondo wa kwanza nyumbani na kurejea nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa, kwa ushindi wa 4-1 dhidi ya Barcelona Jumanne.
PSG ilichukua fursa ya kadi nyekundu ya kipindi cha kwanza kwa mlinzi wa Barcelona Ronaldo Araujo na kusonga mbele kwa jumla ya 6-4 na kufuzu mechi yake ya kwanza katika nusu fainali tangu 2021.
Mshambulizi wa zamani wa Barcelona Ousmane Dembele na Vitinha pia waliifungia PSG baada ya Araujo kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 29 kwa kumchezea vibaya Bradley Barcola na kusimamisha mchezo huo.
Barcelona walikuwa wameanza vyema na wakatangulia kufunga kwa bao la Raphinha dakika ya 12, lakini wageni walichukua udhibiti kwa faida ya mtu na hawakuiruhusu Barcelona kurejea mchezoni.
Bao la Mbappe
Mbappe alifunga mabao yake dakika ya 61 na 89.
Timu hiyo ya Catalan ilifuzu hatua ya mtoano ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuondolewa mara mbili mfululizo katika hatua ya makundi.
Katika robo fainali nyingine Jumanne, Borussia Dortmund iliishinda Atletico Madrid 4- 2 nyumbani na kusonga mbele kwa jumla ya 5-4.