Mwanasoka bora duniani FIFA

Lionel Messi, Erling Haaland na Kylian Mbappe ndio wachezaji waliosalia kutoka jumla ya wachezaji 12 waliteuliwa awali kuwania tuzo ya Mchezaji bora duniani FIFA, baada ya kuchaguliwa na jopo la wataalam.

Kutoka orodha hii fupi, watatu hao walichaguliwa na jopo la kimataifa lililojumuisha: -- -- Makocha wa timu za taifa kwa wanaume, - Nahodha timu za taifa kwa wanaume, - Waandishi wa habari wa soka, - na Mashabiki ambao walipiga kura kwenye wavuti rasmi ya FIFA

Lionel Messi, ambaye alitunukiwa mchezaji bora mwanaume 2022, alirejea kuiongoza Argentina taji la Kombe la Dunia Qatar kwa kusaidia PSG kuinua taji yao ya hivi karibuni ya Ligue 1, ya Pili Ufaransa, huku pia alitajwa katika timu bora ya Ligue 1 ya msimu uliopita.

Messi

Erling Haaland alikuwa na msimu wa kukumbukwa ikiwa ni pamoja na kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora Ulaya, mfungaji bora Premier League pamoja kutangazwa mwanasoka bora wa mwaka Premier League na chipukizi bora wa msimu Premier League.

Erling Haaland

Kwa upande wake, Mbappe alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1 na pia akatawazwa mfungaji Bora wa ligi hiyo.

Mbappe

Mbappe ana mabao manne tu nyuma ya Mfungaji bora wa Kombe la Dunia Fifa Miroslav Klose, huku mchezaji huyo wa Zamani wa Kimataifa wa Ujerumani akiwa amefunga mabao 16 katika michezo 24 katika matoleo manne ya mashindano hayo. Mfaransa huyo mwenye Umri wa miaka 24 tayari ana magoli 12 kati ya mechi 14 alizocheza mwaka wa 2018 na 2022.

Pep Guardiola

Kwa upande wa tuzo za Kocha bora duniani, Pep Guardiola, Simone Inzaghi, na Luciano Spalletti wanawania kutunukiwa kwa kuzisaidia timu zao.

Wakati huo huo, Yassine Bounou, Thibaut Courtois, Ederson wameteuliwa kuwania golkipa bora wa mwaka 2023.

Mshindi wa tuzo hiyo atajulikana rasmi katika sherehe iliyoratibiwa kufanyika London, tarehe 15 Januari 2024.

TRT Afrika na mashirika ya habari