Timu ya kina dada ya Morocco, maarufu ‘Simba jike wa Atlas’, imeweka historia kwa kushuka dimbani Melbourne Rectangular nchini Australia kucheza dhidi ya Ujerumani baada ya kufuzu kushiriki kombe hilo la dunia na kuwa timu ya kwanza kutoka maeneo ya kiarabu kushiriki ngarambe hizo.
Uhodari wa Morocco kufuzu Kombe la dunia, ulianza ilipofika nusu fainali ya WAFCON na kuwa timu ya kwanza ya Afrika kujikatia tikiti. Wenyeji hao wa Kombe lililopita la ubingwa wa Afrika kwa kina dada, 2022, walionyesha ubabe wao dhidi ya wawakilishi wengine wa Afrika walipozifunga Nigeria na Botswana kwenye michuano hayo mjini Rabat na kutinga fainali.
Ingawa ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kufuzu kwa Kombe hilo la Mataifa ya Afrika la CAF kwa Wanawake, Moroko, inayofunzwa na Reynald Pedros, ilicheza mechi13 bila kupoteza hata mechi moja kabla ya kufungwa na Afrika Kusini kwenye fainali.
Aidha, kocha wa timu hiyo, Reynald Pedros alitunukiwa kuwa Kocha Bora wa FIFA wa timu za Wanawake, mnamo mwaka 2018.
Nahodha wa timu hiyo ni Ghizlane Chebbak, mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa kina dada Morocco, ambaye pia ni bintiye nyota wa zamani wa timu ya wanaume ya Morocco, Larbi Chebbak.
Mbali na Ghizlane, Morocco pia inamtegemea Rosella Ayane, mchezaji wa Tottenham Hotspur aliyeamua kuichezea Morocco manmo 2021 licha ya kuiwakilisha Scotland kwenye timu ya wachezaji wasiozidi umri miaka 17 na 19.
"Hatushiriki tu Kombe la Dunia ili kujumuisha nambari. Timu ya wenzetu wanaume wametuonyesha kuwa hakuna kinachoshindikana ikiwa utaipigania na ukikaa umakini. Lengo letu ni kushindana na timu kubwa zaidi kwenye mashindano."
Moroko ilishinda tuzo ya kimataifa ya wanawake ya VisitMalta baada ya ushindi mnono dhidi ya wenyeji Malta (1-0) na Moldova (4-0).
Morocco inayorodheshwa nambari 72 katika timu za taifa za wanawake duniani na FIFA, inachuana na Ujerumani inayoshikilia nambari 2 ulimwenguni. Morocco ilicheza mchezo wake wa kwanza wa soka ya wanawake mwaka wa 1998, na wakati mpinzani wake akiwa na uzoefu na kuzalisha mafanikio.
Morocco ni taifa la kwanza la Afrika Kaskazini na lenye wingi wa Waarabu kufuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake huku ikitumai kuchukua kijiti cha timu yake ya wanaume iliyobeba huko Qatar.
- Tangu 2007, FIFA ilijumuisha hijabu katika orodha ya mavazi iliyopiga marufuku kwa wachezaji hadi kumpelekea Asmahan Mansour kuzuiwa kucheza mechi na Shirikisho la Soka la Quebec kama njia ya kutekeleza marufuku hiyo alipokataa kuvua hijabu yake.
Mnamo 2011, timu ya kina dada ya Iran ilizuiwa kucheza mechi ya kufuzu kwa Olimpiki dhidi ya Jordan kwa sababu ya hijabu zao
FIFA iliondoa marufuku hiyo mnamo 2012 na kuwaruhusu wachezaji kuvaa hijabu ya Kiislamu wakati wa michezo ya soka.
- Aidha, Nouhaila Benzina wa Morocco amekuwa mchezaji wa kwanza wa hijab kucheza kwenye Kombe la Dunia la Soka kwa Wanawake. Shirikisho la soka duniani