Morocco iliibuka na ushindi wa ajabu kwa kuishinda Jamhuri ya Korea 1-0 mjini Adelaide. Timu inayoorodheshwa ya 72 ulimwenguni ilifunga mapema na kushikilia mahasimu wao waliowekwa nafasi 55 juu yao.
'Atlas Lioness' ambao wanacheza kwa mara yao y akwanza kabisa dimba hili walianza kwa mguu wa baraka - na kupata busti ya mapema kwa bao kunako dakika ya 6 tangu mechi kuanza.
Krosi ya Salma Amani ilikutana na mpira mzuri wa kichwa kutoka kwa Ibtissam Jraidi, ambaye alimfukutia kiki la ajabu kipa wa Korea Kim Jungmi na kufunga bao la kwanza kabisa kwa taifa kwenye fainali za kimataifa.
Hata hivyo hakukuwa na uchache kwa Korea kwani mchezo uliendelea kuwanipe nikupe huku timu zote mbili ziliendelea kupata nafasi katika kipindi cha kwanza lakini hakuna aliyeweza kubadilisha. Licha ya kumiliki mpira kwa nguvu kwa Jamhuri ya Korea, shuti lao la kwanza lililolenga goli halikufika hadi baada ya mapumziko.
Moroko waliweza kuwabana Korea hadi kipenga cha mwisho - kuwaacha wanaKorea na majoinzi. Ikiwa Ujerumani itaepuka kushindwa dhidi ya Colombia leo usiku, Korea itaondolewa kutoka Australia na New Zealand 2023.
Mechi yao ya mwisho (Morocco) katika awamu ya makundi wanacheza dhidi ya Colombia Alhamisi 3 Agosti.