Salah ameghadhabishwa na kushindwa kwa Liverpool kufuzu Klabu bingwa ulaya 2024. Anasema hakuna sababu kamwe / Picha: Reuters

Matumaini ya Liverpool kuingia kombe la klabu bingwa Ulaya 2024 yalizimwa Alhamisi baada ya Manchester United kunyakua fursa ya mwisho iliyosalia na kujiunga na Manchester City, Arsenal na Newcastle United

United waliwacharaza Chelsea 4-1 kujishindia nafasi hiyo.

Mchezaji nyota wa Liverpool alieleza katika mtandao wake wa Twitter kuwa wamesikitishwa na matokeo hayo.

“Hatuna kisingizio chochote kwa matokeo haya.’’ Alisema Salah, ambaye amefungia Liverpool magoli 30 tangu kuanza msimu huu. ‘ Tulikuwa na kila tulichohitaji kufuzu shindano hilo na tukashindwa.’

Hii ni mara ya kwanza tangu Salah kujiunga na Liverpool, kukosa kufuzu Kombe la Klabu Bingwa Ulaya.

Kwa upande mwingine Newcastle United wamerudi katika shindano hilo baada yakukosa kwa miaka 20.

TRT Afrika