Kiungo wa Ecuador mwenye umri wa miaka 21, Moises Caicedo amesaini makubaliano ya miaka minane Stamford Bridge, huku klabu hiyo ikiwa na chaguo la kurefusha mkataba huko kwa muda wa mwaka mmoja zaidi.
Kiungo huyo mkabaji amefafanua kuwa usajili wake ni ndoto iliyotimia na hata hawezi kusubiri kuingia uwanjani kuanza na timu ili kuweka historia.
"Nina furaha sana kujiunga na Chelsea! Nina furaha sana kuwa hapa katika klabu hii kubwa na siku lazimika kufikiria mara mbili wakati Chelsea iliponipigia simu, nilijua tu nilitaka kusaini na klabu hiyo." Alijieleza.
Caicedo, ambaye aliwaniwa na Liverpool na Chelsea, kabla ya kuichagua Chelsea, alisema kuwa uamuzi wake wa kuichagua Chelsea unatokana na uhusiano wake na klabu hiyo.
"Nilipokuwa mdogo, nilikuwa shabiki wa Chelsea na nilikuwa nikifuatilia mechi za timu hiyo. Chelsea ni moja kati ya vilabu kubwa duniani." Alisema.
Caicedo aliongeza kuwa amekuwa akitazama mkusanyo wa video za kiungo wa zamani wa Chelsea na Ufaransa, Claude Makelele mtandaoni ili kujifunza uchezaji wake wa nafasi, na uwezo wa kushinda mpira.
Msimu uliopita, Caicedo alituzwa kuwa Mchezaji Bora wa Msimu wa klabu hiyo na Mchezaji Bora wa Msimu wa Wachezaji baada ya kuisaidia klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya sita katika Ligi hiyo alipocheza mechi 43 na kuchangia mafanikio ya klabu hiyo.
Caicedo anakuwa usajili wa kumi wa Chelsea kwenye dirisha hili kufuatia baada ya Christopher Nkunku, Nicolas Jackson, Robert Sanchez, Axel Disasi, Lesley Ugochukwu, Angelo Gabriel, Diego Moreira, Alex Matos na Ishe Samuels-Smith waliotinga Chelsea msimu huu.