Kocha wa Chelsea Pochettino alijizolea sifa kama mmoja wa mameneja wakuu ulimwenguni kipindi kile cha miaka yake mitano akiinoa Spurs kati ya 2014 na 2019.
Aliongoza klabu hiyo kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza kwenye historia yake na kumaliza nafasi ya nne bora kwenye Ligi kuu, premier league, mara kadhaa mfululizo.
Aidha, Spurs hawajawahi kushinda ligi kuu ya Uingereza tangu 1961, Lakini Pochettino anasema lazima wachukuliwe kwa uzito kama washindani.
"Ange (kocha wa sasa wa Spurs) na wafanyikazi wake, wanafanya kazi nzuri na kisha kwa kweli wachezaji wazuri sana, timu nzuri sana," alisema Pochettino. "Unaweza kuhisi wanaweza kuwa wagombea wa taji.
Hata hivyo, kocha wa Spurs, Ange Postecoglou amewataka mashabiki wa Tottenham kumuonyesha heshima Mauricio Pochettino atakaporejea katika klabu yake ya zamani akiwa na Chelsea Jumatatu.
Mkufunzi huyo wa sasa wa Tottenham, Ange Postecoglou ameanza vyema ikilinganishwa na meneja yeyote mpya katika Ligi kuu hiyo baada ya kuchukua pointi 26 kutoka kwa alama 30 katika mechi zake 10 za kwanza katika ligi.
"Sina shaka kutakuwa na kitu chochote isipokuwa heshima kwa Mauricio kutoka kwa mtu yeyote katika klabu hii ya soka, wafuasi au watu wanaohusishwa. Alikaribia kuipeleka klabu hiyo kutwaa Ligi ya Mabingwa, akakaribia kushinda ligi, kwa hivyo kazi yake haina shaka." Ange amemaliza.