Uturuki iliizaba Serbia katika kipute cha kusisimua ya seti tano na kushinda taji la Mashindano ya Voliboli ya Wanawake bara Ulaya, 2023, CEV, siku ya Jumapili.
Timu hiyo ya voliboli ya wanawake ya Uturuki 'Masultan wa wavu' ilishinda fainali kwa seti 27-25, 21-25, 25-22, 22-25, na 15-13 mjini Brussels.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameipongeza Uturuki kwa kushinda kombe hilo.
"Ninaipongeza Timu yetu ya Taifa ya Mpira wa Wavu ya Wanawake, Masultani wa Wavu, kwa kuwa Mabingwa wa Ulaya wa CEV 2023. Wametufanya sote tujivunie," Erdogan alichapisha kwenye mtandao wa kijamii la X.
Vargas alitunukiwa MVP, mchezaji bora zaidi wa Shindano
Melissa Vargas, ambaye aliifungia Uturuki pointi 41 katika mechi hiyo ya fainali, alichaguliwa kuwa "Mchezaji wa Thamani zaidi wa mashindano Ulaya."