Utambulisho huo hutolewa kwa timu na utawala wa UEFA/ Picha: Reuters

Na Kevin Philips Momanyi

Beji ya heshima ya mabingwa barani Ulaya(UEFA) ni hifadhi kwa washindi walio na msimu bora katika dimba hilo, hitaji ambalo mabingwa wapya, Manchester City, bado hawajatimiza.

Beji hii ni picha ya kombe la mabingwa barani Ulaya ambayo huwekwa kwenye bega ya kushoto wa jezi ya klabu ya soka. Nambari inayoonesha klabu imeshinda kombe hilo la mabingwa barani ulaya(UEFA) huandikwa ndani ya beji hiyo.

Utambulisho huo hutolewa kwa timu na utawala wa UEFA. Vilabu vinavyoshinda Ligi ya Mabingwa ya UEFA au UEFA Europa League angalau mara tano katika historia yao au kutwaa kombe hilo mara tatu mfululizo wastahili kupata beji hii ya heshima.

Manchester City ilishinda Ligi ya Mabingwa ya UEFA kwa mara ya kwanza siku ya Jumamosi ilipowalaza Inter Milan 1-0 kwenye Uwanja wa Olimpiki wa Atatürk mjini Istanbul, Uturuki.

Klabu hiyo ya Uingereza italazimika kushinda mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa mara zingine mbili mtawalia au kusubiri kutwaa mara nne zaidi ili kufuzu kupata beji ya heshima ya UEFA.

Hii ina maana kwamba katika msimu ujao wa 2023/2024, mashabiki wa soka duniani kote hawataona beji ya UEFA kwenye mikono ya jezi za wachezaji wa Manchester City.

Kuna timu sita ambazo zinastahili kupata beji hii ya heshima, baada ya kubeba kombe la UEFA angalau mara tano kila moja au kushinda mara tatu mfululizo. Ni Real Madrid (mataji 14; mataji matatu mfululizo), AC Milan (mataji 7), Liverpool (6), Bayern Munich (mataji 6; mataji matatu mfululizo), Barcelona (5).

Ajax Amsterdam, ambayo ina mataji manne ya UEFA, pia ina beji hiyo ya heshima kwa kutwaa taji hilo mara tatu mfululizo, kati ya 1970 na 1973.

Klabu ya Uhispania, Barcelona, imekuwa klabu ya hivi karibuni kutunukiwa beji hii ya heshima baada ya kunyanyua taji lake la tano la UEFA mwaka wa 2015.

Timu nyingine ambazo zina idadi kubwa ya mataji ya UEFA ni Liverpool, Juventus, Inter Milan na Atletico Madrid, ambazo zina mataji matatu kila moja.

Ili kustahiki beji hiyo, timu kama Inter Milan, Manchester United, Juventus, Benfica, na Chelsea pia zitahitaji kushinda Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa angalau mara mbili zaidi.

Mafanikio ya ajabu ya Sevilla, ambao wameshinda Ligi ya Uropa mara saba, yamewapa haki ya kuvaa beji hii ya heshima ya UEFA.

Lakini kwa sasa, hii haitakuwa na maana kwa kocha wa Manchester City Pep Guardiola, wachezaji wake, au wafuasi wa timu hiyo kwani bado wamezama katika shamra shamra za ushindi wao wa jana.

TRT Afrika