Burkina Faso walinyakua fursa baada ya makosa mengi kutoka kwa timu ya Golden Eaglets ya Nigeria ya kupoteza mabao.
Mabingwa hao mara tano wa kombe hilo walibanduliwa kwa 2-0 kwa kuonesha ulegevu katika ‘safu yao ya ulinzi’ iliyojaa mapengo na kuwezesha Junior Stallions kuwashambulia bila huruma.
Charles Agada alijitahidi kadri ya uwezo wake lakini mara mbili, kipa wa kiburkinabe alimuonea mbali na ana kwa ana, aliweza ku ‘bloki’ majaribio yake yote.
Dakika kumi tu baada ya kuanza nusu fainali ya pili Aboubakar Camara alimsukumizia kipa wa Nigeria mkwaju wa penalty baada ya m-nigeria Ogboji kumchezea rafu mshambuliaji Souleymane Alio ndani ya ‘box.’
Sasa Burkina Faso wanapenya nusu fainali na kujinyakulia tikiti ya kombe la dunia la wachezaji wasiozidi miaka 17.
Kwa upande wake Mali, haikulazimika kutoa jasho kwani walielea kwa wepesi sana dhidi ya Congo kwa mabao 3-0.
Nyota waliong’aa katika mechi hiyo ni Ange Tia, Mohamoud Barry na Mamadou Doumbia waliotikisa wavu wa Congo na kuwalazimu kurudi nyumbani na kuzima matumaini yao ya kushiriki kombe la dunia baadaye mwaka huu.
Mechi za nusu fainali zitachezwa Jumapili 14 mjini Algiers ambapo Morocco itachuana na Mali huku Burkina Faso wakikutana na Senegal.
Washindi kutoka mechi hizo mbili watakutana katika fainali, katika uwanja wa Nelsona Mandela mjini Algiers tarehe 19 Mei.