Wawakilishi wa Afrika Mashariki kutoka eneo la CECAFA, JKT Queens ya Tanzania waliifunga CBE FC ya Ethiopia na kufuzu Ligi hiyo ya Mabingwa ya Wanawake CAF. Picha: CECAFA

Droo rasmi ya Ligi ya mabingwa ya soka kwa Wanawake ya CAF, itafanyika jumatatu 09 Oktoba Mjini Abidjan, Cote D'ivoire 2023.

Macho yote yatakuwa ni kwa watakaokuwa wapinzani wa JKT Queens ya Tanzania amabao walijikatia tiketi ya kuiwakilisha Afrika Mashariki kwenye droo baada ya kuifunga CBE FC ya Ethiopia na kufuzu kwa Ligi hiyo ya Mabingwa ya wanawake CAF.

Makala ya tatu ya mashindano hayo ya kifahari ya klabu bora ya wanawake Afrika yatafanyika Cote d'ivoire kati ya tarehe 05 na 19 Novemba 2023, na ndio mara yake ya kwanza kwa mashindano hayo ya klabu ya bingwa wanawake CAF kuandaliwa eneo la Afrika Magharibi.

Klabu zilizothibitishwa kushiriki kwenye ligi ya Mabingwa ya Wanawake CAF, Cote D'ivoire 2023:

  • AS FAR - Morocco (mabingwa watetezi)
  • Athlético Abidjan - Côte d'Ivoire (wenyeji)
  • SC Casablanca - Morocco (wawakilishi wa Afrika Kaskazini)
  • AS And - Mali (wawakilishi wa Afrika Magharibi A)
  • Ampem Darkoa - Ghana (wawakilishi wa Afrika magharibi B)
  • JKT Queens - Tanzania (wawakilishi wa Afrika Mashariki - CECAFA)
  • Mamelodi Sundowns - Afrika Kusini (wawakilishi wa Afrika kusini, na mabingwa 2021)
  • Huracanes - Equatorial Guinea (wawakilishi wa Afrika ya Kati)

AS FAR ya Morocco ndio mabingwa watetezi wa dimba hilo la Ligi ya mabingwa ya Wanawake ya CAF baada ya kuichabanga Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini mjini Rabat mwaka jana.

TRT Afrika