JKT Queens Tanzania

Klabu ya soka ya Wanawake kutoka Tanzania, JKT Queens imewashangaza wengi siku ya Jumatano jioni baada ya kurejea kutoka nyuma ikiwa goli moja chini na kushinda 2-1 dhidi ya wenyeji, Athletico Abidjan, katika raundi ya pili ya mechi za makundi katika Ligi ya Mabingwa ya wanawake ya CAF inayoendelea.

Watanzania walifufua matumaini yao katika Kombe hilo baada ya awali kupoteza dhidi Ya Mamelodi Sundowns, kwa kusajili ushindi muhimu dhidi ya Athletico Abidjan kwenye mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Amadou gon Coulibaly huko Korhogo.

Nguvu mpya Winifreda Gerald, ambaye aliingia kipindi cha pili, aliisawazishia JKT Queens kunako dakika ya 66 kabla ya Alia Salum, mchezaji mwingine aliyeingia kipindi cha pili, aliwashangaza wenyeji hao kwa bao lake la dakika ya 85 ili kuwapa upande wake ushindi huo muhimu.

TRT Afrika na mashirika ya habari