Mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia la Raga itakuwa kati ya wenyeji Ufaransa dhidi ya New Zealand 'All blacks' kwenye Uwanja wa Stade de France Ijumaa, 8 Septemba.
Kwa jumla, mechi 48 zitachezwa kwa muda wa takriban miezi miwili.
Michuano ya kukumbukwa yatahusisha timu za wanaume kwa wachezaji yaani 15s, huku Kombe hilo la Dunia la Raga 2023 likishirikisha jumla ya timu 20.
Timu 12 zilifuzu moja kwa moja kwa kumaliza katika nafasi tatu za juu kwenye kundi lao huko Japan 2019 na nane kutoka kwa mchakato wa kufuzu kimataifa.
Kombe hilo la dunia ambalo ni makala ya 10 ya Raga duniani kwa wanaume, linarejea Ufaransa kwa mara ya pili tangu kuandaliwa nchini humo mnamo 2007 na kuwa shindano la kukata na shoka.
Ngarambe za Dunia za Raga 2023 zitafanyika ndani ya mwaka ambao mchezo huo unaadhimisha miaka 200 tangu kuanzishwa kwake na William Webb Ellis aliyesifiwa kwa kuvumbua mchezo wa raga kwa kuonyesha "kukiuka sheria" katika kudaka mpira na kukimbia nao mnamo 1823.
Hii ni mara ya nane kwa Ufaransa na New Zealand kukutana katika Kombe la Dunia la Raga.
All Blacks wameshinda mechi tano kati ya saba za awali - ikiwa ni pamoja na fainali za mashindano yote ya 1987 na 2011, na robo fainali ya dimba la 2015 walipoingia ndani ya alama tatu za kuandikisha ushindi wao mkubwa kuwahi kutokea dhidi ya Les Bleus.
Kundi A: Ufaransa, Italy, Namibia, New Zealand na Uruguay
Kundi B: Ireland, Romania,Scotland, Afrika Kusini, Tonga
Kundi C: Australia, Fiji, Georgia, Ureno, Wales
Kundi D: Argentina, Chile, England, Japan, Samoa