Na Lynn Wachira
Katika ubora wake, Jean Sseninde angejiweka kwenye mstari wa mbele kulinda goli la soka la wanawake. Kwa hivyo, anapokiri kwamba "Afrika bado haijakumbatia soka ya wanawake", unajua imemchukua muda wa mazingatio beki huyo wa zamani wa Crested Cranes na Queens Park Rangers kuruhusu moja kupita.
Kukiri kwa wazi kwa Sseninde kuwa Afrika imezembea katika kuendeleza mchezo wa wanawake kunakuja kufuatia mkesha wa Kombe la Dunia la Wanawake la FIFA 2023 linalofanyika nchini Australia na New Zealand, kuanzia Julai 20.
Timu nne za Afrika ambazo ni - Morocco, Zambia, Afrika Kusini na Nigeria - zinachuana kuwania kombe katika makala haya ya michuano hiyo, lakini nyota huyo wa zamani wa Uganda anaamini itakuwa vigumu kwa Afrika kutwaa taji hilo kutokana na kukabiliana na nchi zilizopiga hatua kwa kasi katika mchezo huo, ikilinganishwa na "kasi ya konokono" ambayo bara limepiga hatua. Sseninde anapaswa kujua.
Alipotua Uingereza kutoka Uganda akiwa na umri wa miaka 20, aligundua haraka kwamba soka la wanawake ulikuwa ni mchezo mpya kabisa wa mpira. "Nilishangaa nilipoona kwamba soka la wanawake nchini Uingereza lilikuwa kubwa na lenye ushawishi wa kutosha na mara nyingine lilirushwa kwenye televisheni hata wakati huo, huku hakuna aliyezungumza kuhusu kile tulichokuwa tukifanya Uganda," anaiambia TRT Afrika.
"Nilishangazwa kuona wasichana wadogo kabisa kama wanne wakifanya mazoezi na kufanya mambo makubwa na kuonyesha viwango vikubwa uwanjani, ambapo sikuamini macho yangu." Anaambia TRT Afrika.
Uingereza inasalia kuwa taifa la mfano katika kuendeleza soka la wanawake, likiwa na miundo imara ya vijana na ligi.
Ligi Kuu ya Wanawake huko ni ya pili baada ya Ligi ya Kitaifa ya Soka ya Wanawake nchini Marekani. Sseninde alitambulika zaidi kwa kufundisha mpira wa miguu katika shule moja, takriban miaka minne kabla ya mafanikio yake ambayo yalimfikisha kusaini mkataba wa kitaalam na Charlton Athletic WFC mnamo 2012.
"Wachezaji wadogo zaidi kuliko mimi walikuwa bora zaidi kimbinu, na ilinibidi kucheza sana," anakumbuka. Kwa kasi ya miaka 10 baadaye, na Sseninde amerejea kusaidia kuendeleza soka ya wanawake katika nchi yake ya Uganda.
Lakini kasi ambayo hii inafanyika inamsumbua Kutokana na kukosa sapoti. Sio tu Uganda, bali katika bara zima.
"Mabingwa wa dunia walioanza kabla yetu kwa sasa wanaingiza faida tayari kutokana na mchezo huo," anasema Sseninde, ambaye sasa ni mkufunzi wa UEFA mwenye leseni B na anaendesha Taasisi iitwayo Jean Sseninde ambayo imeangazia kukuza vipaji kutoka mashindano yanayofanyika nchini Uganda.
Nafasi ya Afrika
Droo ya timu 32 ya Kombe la Wanawake kwa Afrika, Afrika Kusini, Nigeria ndio angalau zinafanya vizuri kwenye makundi yao Morocco na Zambia zikiwa katika nafasi ya chini zaidi katika makundi yao.
Afrika Kusini ndio mabingwa wa sasa wa Afrika, wakiwa na rekodi nzuri katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake, lakini Super Falcons kutoka Nigeria ndio wenye uzoefu zaidi. Falcons, waliofuzu robo fainali katika Kombe la Dunia la Wanawake la mwaka 1999, watakuwa wakicheza mechi yao ya tisa kwenye michuano hiyo, baada ya kuanza mwaka 1991.
Wakati uzoefu ukizingatiwa katika kiwango cha juu, fomu ya hivi karibuni ya Nigeria imeacha historia ya peke yake kutokana na kiwango kikubwa wanachoonesha. Ingawa wameorodheshwa katika nafasi ya 40 na FIFA.
Super Falcons wanapaswa kukabiliana na ukweli wa kuwa mkiani mwa Kundi B, ambapo watamenyana na Canada (ya 7 duniani), wenyeji Australia (ya 20 duniani) na Ireland (ya 22 duniani). Katika safu zao, Super Falcons wana Asisat Oshoala, fowadi wa Barcelona Femeni ambaye ameorodheshwa na FIFA kama mmoja wa nyota watano wa kuangaliwa kwenye Kombe la Dunia.
Pia kuna Onome Ebi, nahodha wa timu hiyo na mwanasoka pekee wa Kiafrika - kujumuishwa sehemu ya Kombe la Dunia la sita. Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Rasheedat Ajibade, ni nyota mwingine anayetarajiwa kuwasha moto kwenye mashindano hayo.
Afrika Kusini, inayoitwa Banyana Banyana, hatimaye iliwaondoa Super Falcons kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake mwaka jana baada ya kumaliza nafasi ya pili mara tano na nafasi ya tatu mara mbili. Katika mechi yao ya awali ya Kombe la Dunia mwaka 2019, Afrika Kusini haikufuzu hatua ya makundi.
Desiree Ellis na kikosi chake watamenyana na Sweden, Argentina na Italia waliofuzu kwa nusu fainali 2019 katika Kundi B, huku Thembi Kgatlana akiwa mchezaji nyota wa kuangaliwa katika timu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliifungia Banyana Banyana bao pekee la Kombe la Dunia walipocheza dhidi ya Uhispania mnamo mwaka 2019.
Morocco ilikuwa mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake 2022 na kufika fainali yao ya kwanza, ikiangukia pua na kupata kipigo kutoka kwa Afrika Kusini. Atlas Lionesses wanaonekana kuwa timu inayokua kwa kasi katika mchezo wa wanawake.
Wakiwa wameorodheshwa katika nafasi ya 72 na FIFA, Atlas Lionesses wanaweza kupata msukumo kutoka kwa chachu iliyooneshwa na timu ya wanaume ya Morocco iliyofika hadi nusu fainali ya kwenye Kombe la Dunia la FIFA la 2022 nchini Qatar.
Fowadi wa Tottenham Hotspur, Rosella Ayane, ndiye atakayeongoza safu ya mashambulizi ya Morocco. Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England chini ya umri wa miaka 19 yuko katika hali nzuri, akifunga mabao saba katika mechi 15 zilizopita. Copper Queens ya Zambia, ambao pia walishiriki Olimpiki ya Tokyo 2020, sio wadhaifu pia.
Wakiongozwa na Barbra Banda mchezaji hatari, kichapo chao cha kushangaza cha 3-2 kutoka kwa mabingwa mara mbili wa dunia Ujerumani kwenye uwanja wa nyumbani hivi majuzi kimeibua matarajio yao makubwa au mawili kwenye Kombe la Dunia.
Barbra, mwenye umri wa miaka 23, alivutia umati wa kimataifa alipokuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick za mfululizo kwenye Olimpiki. Dhidi ya Ujerumani, mabao mawili yaliacha wenyeji wakiwa wameshtuka.
Copper Queens ndio timu iliyo katika nafasi ya chini zaidi ya michuano hiyo ikiwa katika nafasi ya 77, na wamepangwa Kundi C pamoja na Uhispania (ya 6 duniani), Japan (ya 11 Duniani ) na Costa Rica (ya 36 duniani).
Mwamko mpya
Kipindi hiki mchezaji gwiji Sseninde anazishauri timu zote nne za Afrika katika droo iliyopangwa ya Kombe la Dunia kutumia mashindano hayo kama msukumo na fursa ya kuendeleza mchezo huo Barani Afrika.
"Unaweza kusema kwamba safari hii ni mashindano yaliyokuwa kaa Kiasi; kwa hivyo, kila mtu anaweza kujitokeza na kuonyesha kipaji. Wakati huo huo, ni fursa yetu kuwa na timu nne uwanjani, na tunapaswa kuitumia kwa busara na timu hizi zinaweza kuonyesha kuwa Afrika tunaweza," anasema beki huyo mstaafu.
"Tutatazama wachezaji wengi wa Kiafrika wakiwahamasisha wasichana wetu wadogo kucheza mpira wa miguu, huku wazazi na wafadhili wengi wakielewa kuwa soka la wanawake lina nafasi barani Afrika."
Mchezaji huyo wa zamani wa Charlton Athletic pia anatoa wito kwa wale ambao wamefanikiwa katika mchezo huo kutoka Afrika kurudi kwenye nchi zao na kuwasaidia wasichana wachanga kufika kwenye kiwango cha juu.
"Kusema kweli, mpira wa miguu wa wanawake bado haujakubaliwa kikamilifu barani Afrika kwa kiwango tunachohitaji, wadau wengi bado wanaona ushiriki wao katika mchezo kama neema, unazuia uwekezaji wa kweli katika mchezo."
Anatoa mfano wa mvutano wa hivi majuzi wa malipo kati ya Banyana Banyana na Chama cha Soka cha Afrika Kusini ambao ulishuhudia timu hiyo ikisusia mechi ya kirafiki dhidi ya Botswana.
"Ilikuwa bahati mbaya kuona kutajwa kwa majina dhidi ya Banyana hata na viongozi wa soka. Malalamiko ya wanasoka wa kiume daima yamechukuliwa kwa uzito, huku wanawake wanaojitetea wanaonekana kukosa heshima," alieleza Sseninde.
Tunatarajiwa kuchukua chochote tunachopewa, kutii kila wakati, na kukaa kimya. Ninawahimiza wanawake kuendelea kupigana na kusimama wenyewe haki zao ili kuifanya kesho Yao iwe bora zaidi kwa wasichana wadogo wa Kiafrika wenye ndoto ya mafanikio ya soka."
Kando na malipo duni, soka la wanawake barani Afrika linaendelea kugubikwa na madai ya unyanyasaji wa kijinsia, huku kocha mkuu wa Copper Queens Bruce Mwape akikabiliwa na mashtaka ya utovu wa nidhamu.
Lakini licha ya vizingiti vyote, Afrika bado inatazamia kushangilia timu zake nchini Australia na New Zealand huku kandanda la wanawake na mashabiki katika bara zima wakisubiri kwa hamu mafanikio ya Timu za Afrika.