Karim Benzema atahamia Saudi Arabia kujiunga na Al Ittihad. / Picha: AFP

Taarifa kwenye tovuti ya klabu ya Real Madrid Jumapili ilitangaza rasmi kuondoka kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 na kumtaja kama "mchezaji mkuu katika enzi hii ya historia yetu."

Karim Benzema atahamia Saudi Arabia kujiunga na Al Ittihad. Benzema mwenye umri wa miaka 35 alikaa kwa misimu 14 Bernabeu ambapo alishinda Ligi ya Mabingwa mara tano, ubingwa wa LaLiga manne, na Ballon d'Or 2022.

Mnamo Januari, Benzema alipokea mkataba sawa na ya Cristiano Ronaldo, aliyesajiliwa na Al Nassr, kwa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Euro milioni 400.

Real Madrid sasa wamefahamisha kuwa hafla ya kumwaaga itafanyika Jumanne, huku rais wa klabu hiyo Florentino Perez akitarajiwa kuhudhuria

Mnamo 2009, Benzema, mmoja wa washambuliaji bora chipukizi wa Uropa, alihamia Madrid kutoka Lyon na kuwa mfungaji bora wa pili wa klabu hiyo katika historia ya Real Madrid. Kabla ya kujiunga na kikosi cha Real Madrid, alilazimika kupigania nafasi hiyo na Gonzalo Higuain.

TRT Afrika