Jude Bellingham asherehekea ushindi wa Real Madrid dhidi ya FC Barcelona kenya mechi ya debi la ligi, "El clasico". Picha Getty

Katika mechi ambayo ilianza kwa mdundo wa Rolling Stones, ambapo wanamziki maarufu Mick Jagger na Ron Wood wakiwa miongoni mwa mashabiki, Barcelona iliweza kuchukua uongozi dhidi ya Real Madrid, ambayo ilirejea kwa mpigo katika awamu ya pili.

Barça ilichukua uongozi kupitia bao la mapema lililofungwa na Mjerumani Ilkay Gundogan dakika ya (7), baada ya pasi kutoka Ferran Torres kabla ya mabeki wa Madrid kujikanganya na kumpa Gundogan uwezo wa kuelekeza wavu langoni dhidi ya mlinda lango Kepa na kufanya mechi iwe1-0.

Hata hivyo, katika kipindi cha pili, Bellingham alisawazisha kwa kombora ndefu katika dakika ya (68) kabla ya kuinyakulia Madrid ushindi wa 2-1 muda wa nyongeza (90+2), na hivyo kuiwezesha Real Madrid kusalia juu ya msimamo wa ligi.

Mwingereza huyo alifyatua risasi kali sana kutoka mbele hadi kumduwaza kipa Ter Stegen (68).

Kiungo huyo wa Uingereza, Bellingham, anaendelea kuwa tegemeo la timu yake huku akizidi kuongeza idadi ya mabao yake ili kujiimarisha kama mfungaji bora wa ligi kuu ya Uhispania akiwa na mabao kumi.

Goli hilo liliwaweka wenyeji hao mbele na kusababisha wasiwasi kwa Real Madrid, ambayo ilionekana kutokuwa na wasiwasi juu ya bao la mpinzani katika dakika 45 za kwanza.

Mchuano huo pia ulishuhudia ubabe kati ya Bellingham na kiungo wa Barcelona Gavi, huku naye nyota wa Brazil Vinicius akikatwa makali na beki wa Uruguay Ronald Araujo.

Barcelona ilikuwa hatari zaidi, hasa kwenye wingi la kushoto ambapo Mreno Joao Felix na Mhispania Alejandro Balde walimtatiza Dani Carvajal na kuwa kibarua kwake.

Kufuatia ushindi huo, Real Madrid, maarufu Los Merengues wamefanikiwa kudumisha uongozi wao wa ligi wakiwa na pointi 28, ingawa ni pointi sawa na klabu ya Girona, huku Barcelona ikibaki katika nafasi ya tatu, ikiwa na pointi 24, pointi nne nyuma ya Real Madrid.

AFP