Miamba hao wa Ukraine waliisukuma Barcelona hadi mwisho mechi iliyotangulia ikiwa ndio mchezo wa kwanza wa kocha mpya Marina Pusić ambaye pia anaamini wanatoshana nguvu na Barcelona.
"Kila mechi ina nguvu yake yenyewe. Sidhani kama mechi ya mwisho dhidi ya Barcelona itakuwa sawa na hii. Tunaweza kushindana nao. Tumekuwa na wakati wa kufanya kazi pamoja. Ni mechi ya nyumbani, lakini sio mechi ya nyumbani hata kidogo. Tumetumia muda mwingi kusafiri. Sio rahisi kwetu, lakini hatuko hapa kulalamika,” Marina Pusić alisema.
Miroshi, beki wa kushoto anayetegemewa na timu hiyo na taifa stars ya Tanzania, mwenye umri wa miaka 21, ameshirikishwa kwenye kikosi kilichosafiri kuelekea Ujerumani ambapo uwanja wa Volksparkstadion, Hamburg, ndio uwanja wao wa nyumbani kwa muda.
Kuna uwezekano Miroshi akajaza mojawapo ya nafasi za wachezaji wa Shakhtar Bondarenko and Konoplya waliodhibitiwa kutoshiriki mechi hiyo.
Macho ya mashabiki wa soka Tanzania na Afrika Mashariki yanatarajiwa kuelekezwa uwanjani Volksparkstadion, usiku huu wakati chipukizi Miroshi na wenzake watakapokwaruzana na Barcelona ya Uhispania.
Miroshi alijiunga na Shakhtar Donetsk kwa njia ya mkopo kutoka Zulte Waregem, ya ligi kuu ya soka nchini Ubelgiji.