Jurgen Klopp, mmoja wa makocha waliofanikiwa zaidi Liverpool, anaondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu akisema anaishiwa nguvu.
"Ninapenda kila kitu kuhusu klabu hii, napenda kila kitu kuhusu jiji, napenda kila kitu kuhusu wafuasi wetu, ninaipenda timu, ninawapenda wafanyakazi," Klopp alisema katika mahojiano marefu kwenye tovuti ya timu hiyo. "Ninapenda kila kitu.
"Lakini kwa kuwa bado nachukua uamuzi huu inakuonyesha kwamba nina hakika kuwa ndio ninayopaswa kuchukua. Ni kwamba ... ninaishiwa na nguvu. Najua kwamba siwezi kuifanya kazi hiyo tena na tena na tena na tena."
Tangazo la mshtuko la meneja huyo mwenye umri wa miaka 56 linakuja baada ya Liverpool kutinga fainali ya Kombe la Ligi siku ya Jumatano na katikati ya msimu ambao timu yake iko kwenye mbio za kuwania mataji manne na kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Kazi yenye mafanikio
"Baada ya miaka ambayo tulikuwa pamoja na baada ya muda wote tulioishi pamoja na baada ya mambo yote tuliyopitia pamoja, heshima ilikua kwako, upendo uliongezeka kwako na deni langu kubwa kwako ni ukweli - na hiyo ndiyo dhamana. ukweli,” alisema.
Mjerumani huyo alijiunga na Liverpool Oktoba 2015 na ameshinda Ligi ya Mabingwa, Ligi Kuu, Kombe la Dunia la Klabu, Kombe la FA, Kombe la Ligi na Kombe la Super Cup, pamoja na Ngao ya Jamii wakati alipokuwa kocha.
Klopp ana kiwango cha juu zaidi cha ushindi kuliko meneja yeyote katika historia ya Liverpool katika mashindano yote kwa 60.7% na ndiye meneja pekee aliyeshinda kila Ligi ya Premia, Ligi ya Mabingwa, Kombe la FA na Kombe la Ligi.
Aliiongoza Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa mnamo 2019, na taji la ligi mwaka mmoja baadaye, la kwanza katika miaka 30 na la kwanza la enzi ya Ligi Kuu.
Hakuna hofu kwa afy ayake
Alipoulizwa kama anaondoka kwa sababu za kiafya, Klopp alisema: "Mimi ni mzima wa afya, kadiri unavyoweza (kuwa) katika umri wangu."
Klopp alisema alivutiwa na wazo la kuondoka mnamo Novemba wakati akikutana na kilabu kuhusu wachezaji wanaoweza kusajiliwa na kambi ya msimu ujao wa joto.
"Kwangu mimi ilikuwa muhimu sana, muhimu sana kwamba naweza kusaidia kurudisha timu hii kwenye reli.
"Siyo ninachotaka (kufanya), ni kile ninachofikiri ni sawa kwa asilimia 100. Ndivyo hivyo."
Klopp alisema katika ulimwengu mzuri angesubiri hadi mwisho wa msimu kutangaza kuondoka kwake, lakini haiwezekani "kuweka mambo kama haya kuwa siri". Alisema baada ya "nyuso chache za huzuni kwa siku chache" anatumai timu inaweza kurejea kwenye kazi yake kama kawaida.
Alipoulizwa kuhusu mwitikio wa klabu, alisema "Hawakupiga sherehe!"