Kipande cha video kilichogusa hisia kimejitokeza wiki hii na kimeangaliwa na watu wengi mitandaoni na kusababisha madai ya ubaguzi wa rangi dhidi ya utawala wa michezo huo nchini Ireland.
Tukio hio ilitokea kwenye hafla ya Gymstart katika mji mkuu wa Ireland mwezi Machi mwaka jana na video inaonyesha safu ya watoto wote wakipewa medali isipokuwa msichana mweusi pekee, ambaye alipuuzwa na makocha wake.
Taarifa, ya tarehe 25 Septemba, kutoka Gymnastics Ireland inasema: "Kwa niaba ya Bodi na wafanyakazi wa Gymnastics Ireland tungependa kuomba radhi bila masharti kwa mwanamazoezi na familia yake kwa masikitiko yaliyosababishwa na tukio hilo kwenye hafla ya GymStart mwezi Machi 2022. Kilichotokea siku hiyo hakikufaa kutokea na kwa hilo tunasikitika sana."
Mwaka na zaidi bila kuomba radhi
Hii inakuja baada ya mama wa mwanamazoezi kunukuliwa na gazeti la Irish Independent Jumapili akisema kuwa hawajapokea msamaha bado kutoka Gymnastics Ireland na kwamba amepeleka suala hilo kwa Gymnastics Ethics Foundation, shirika linalosimamia utaratibu wa maadili kwenye michezo hayo, huko Uswisi.
Gazeti hilo pia liliarifu kwamba familia inaamini binti yao alipuuzwa kwenye sherehe hiyo kwa sababu alikuwa mweusi.
"Uwa tunakuwa familia pekee weusi kwenye hafla za mazoezi ya viungo na hili limetuuma sana," mama aliliambia gazeti hilo.