Nigeria ilitoka Sare 0-0 mechi ya ufunguzi dhidi ya Canada kisha wakashinda dhidi ya Australia 3-2 na sasa tena 0-0 dhidi ya Ireland Picha : Super Falcons Twitter 

Nigeria imefuzu kwa awamu ya muondoano ya Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake kwa mara ya tatu baada ya kutoka sare ya 0-0 na Jamhuri ya Ireland siku ya Jumatatu.

Hatima ya Ireland ilifungwa kabla ya mchezo huu baada ya kushindwa vibaya na Australia na Canada - lakini msuguano na Super Falcons uliwafanya wachukue pointi ya kwanza kabisa ya Kombe la Dunia la Wanawake.

Nigeria itaungana na Australia katika hatua ya 16 bora, huku wenyeji wenza wakiwapeleka mabingwa wa Olimpiki Canada nyumbani kufuatia ushindi mnono wa mabao 4-0.

Nigeria itaungana na Australia katika hatua ya 16 bora, Picha Twitter Super Falcon

Mojawapo ya matukio ya kukumbukwa zaidi ya mchezo huo ilikuja baada ya muda mfupi, wakati kipa wa Ireland Courtney Brosnan alipotoa zima mkwaju wa kinajiera na kuokoa jahazi upande wake.

Uchenna Kanu alijaribu kugusa kwa kichwa pasi ya Toni Payne ndani ya eneo la goli, lakini mpira wake wa kichwa ukapanguliwa kwenye eneo la goli kutoka kwa Brosnan, ambaye alishuka haraka ili kumfukia chini.

Kata, Pasua!!! Juhudi zote za Nigeria ziliambulia patupu licha ya kijasho walichotoa kutafuta ushindi.

Beki wa Nigeria Onome Ebi amekuwa mwanasoka wa kwanza wa Kiafrika - wa kiume au wa kike - kucheza katika Kombe la Dunia mara sita.

TRT Afrika