Mashabiki wa Valencia wakiimba "Mono" (tumbili) kuelekea Vinicius | Picha: AA

Polisi wa Uhispania waliwashikilia watu saba Jumanne kwa tuhuma za uhalifu na ubaguzi na chuki unaomlenga mchezaji wa Real Madrid, Vinicius Jr, huku ligi kuu ya soka ya Uhispania ikihimiza mabadiliko ya sheria ya Uhispania ambayo yataiwezesha kuchukua hatua za kukomesha ubaguzi wa rangi viwanjani.

Watu watatu wameshikiliwa mjini Valencia wakihusishwa na kashfa za ubaguzi wa rangi alizotupiwa Mbrazil huyo wakati wa mchezo wa LaLiga Jumapili.

Wengine walikamatwa huko Madrid, na wanatuhumiwa kwa kutundika sanamu ya nyota huyo kwenye daraja.

Shirikisho la soka la Uhispania pia lilichukua hatua siku ya Jumanne.

Imebatilisha kadi nyekundu ambayo Vinicius alipokea wakati wa mechi ya Jumapili, na imeipiga faini ya takriban dola elfu 50 kwa klabu hiyoy Valencia

Uwanja wa Valencia, ambako unyanyasaji huo ulianzia, pia itafungwa kwa mechi tano.

Tukio hilo linaangazia jinsi ubaguzi wa rangi unavyosalia kuwa tatizo katika soka. Lakini La Liga - ligi kuu ya soka ya Uhispania - inasema mikono yake imefungwa.

Inasema kuwa sheria ya Uhispania inaiwekea vikwazo kuwa na uwezo wa kushughulikia suala hilo, kwani inaweza tu kugundua na kuripoti matukio ya ubaguzi. na anatoa wito kwa mamlaka ya kufuta mechi na kupiga marufuku mashabiki kutoka viwanjani.

Wakati huo huo, makumi ya wanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi wamekuwa wakikusanyika nje ya ubalozi mdogo wa Uhispania huko Sao Paulo.

Waliimba nyimbo za kumuunga mkono Vinicius na kushutumu LaLiga kwa ubaguzi wa rangi.

Reuters