Vilabu vya soka vya Uturuki vimeandikisha mafanikio makubwa huku "Big Three" (Timu tatu bora) katika soka la Uturuki wakitinga hatua ya makundi katika mashindano ya vilabu bingwa UEFA.
Kwenye msimu wa 2023-24, Galatasaray, Fenerbahce, Besiktas, na Yukatel Adana Demirspor kwa jumla walipata ushindi katika mechi 20 kati ya 24 walizocheza.
Hata hivyo, ilikuwa hali tofauti kwa timu nyingine ya Uturuki, Yukatel Adana Demirspor, ambayo iliaga mashindano ya Ulaya baada ya kutimuliwa kupitia mikwaju ya penalti katika hatua ya mchujo.
Kufuatia usajili wake wa ushindi 20 na sare mbili, Uturuki ilitoka nafasi ya 13 hadi nafasi ya tisa kwenye orodha ya UEFA kabla ya awamu ya makundi kwa matokeo haya.
Galatasaray imefuzu kwa mara 17
Galatasaray ilijizolea ushindi mara tano na sare moja katika mechi zake sita za kufuzu na kujihakikishia tiketi kwa mara 17 katika harakati zake za kushirki Ligi ya Mabingwa.
Katika hatua ya makundi, Galatasaray ilipangwa katika Kundi A pamoja na Wajerumani Bayern Munich kutoka Bundesliga na mashetani wekundu wa Manchester United kutoka Ligi Kuu ya England na Copenhagen ya Denmark.
Klabu ya kandanda ilifuzu kwa hatua ya makundi kwa kuwashinda Zalgiris, Olimpija Ljubljana, na Molde, mtawalia.
UEFA Conference League
Jumla ya vilabu vitatu kutoka Ligi Kuu ya Uturuki viliiwakilisha Uturuki katika kiwango cha kufuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Conference.
Fenerbahce na Besiktas walifika hatua ya makundi baada ya kuwatandika wapinzani wao, huku Adana Demirspor ikiaga Ligi ya Conference baada ya kupoteza kwa njia ya mikwaju ya penalti dhidi ya Genk ya Ubelgiji.
Fenerbahce waliwazamisha Zimbru, Maribor, na Twente, huku Besiktas ikiikwatua Tirana, Neftci Baku, na FK Dinamo Kiev na kujihakikishia nafasi ndani ya hatua ya makundi.
Kutokana na alama hizi, Uturuki ilikusanya 32,850 na kushika nafasi ya tisa katika orodha ya UEFA.