Mabingwa wapya wa Afrika, Côte D'ivoire wanashika nafasi ya 10 na ya 39, Afrika na Duniani mtawalia, kulingana na orodha mpya iliyotolewa na Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Duniani(FIFA).
Hatua hii inafuatia mafanikio wa 'Tembo' hao walioitwaa taji la AFCON 2023 kwenye ardhi yao hivi karibuni.
Wakati huo huo, Nigeria iliyomaliza katika nafasi ya pili, imechupa hadi nambari 28 duniani kwa kupanda nafasi 14.
Afrika Kusini ni mojawapo ya mataifa mengine yenye mafanikio ya kujivunia kwani imepanda na kukamata nafasi ya 10 barani Afrika.
Aidha, Taifa stars ya Tanzania imepanda nafasi mbili juu huku kutoka 121 hadi 119.
DRC iliyomaliza katika nafasi ya nne kwenye michuano hiyo, inashika nafasi ya 12 Afrika, baada ya kukwea hatua nne juu.
Uganda imesalia katika nafasi ya 92 huku Harambee Stars ya Kenya ikizama nambari 111.