Cristiano Ronaldo anaongoza kwenye orodha ya Forbes ya wanasoka 10 waliolipwa zaidi mwaka 2023 akikusanya mapato ya ndani na nje ya uwanja ya $136 milioni.
"Ronaldo anaongoza kwa kuzoa wastani wa dola milioni 136, zikiwemo dola milioni 46 kutoka kwenye mshahara wake wa kucheza na bonasi na $ 90 milioni kutokana na mwonekano, mapato ya leseni na juhudi zingine za biashara," Forbes ilisema kwenye tovuti yake.
Ronaldo, 38, aliondoka Manchester United mwezi Novemba na kuelekea Al-Nassr ya Saudi Arabia mwezi Januari ili kuongeza mapato yake.
Nyota huyo wa kandanda aliichezea Ureno timu yake ya taifa katika Kombe la Dunia la FIFA la 2022 ambalo lilinyakuliwa na Argentina.
Ronaldo, mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Juventus na Manchester United, alishinda mataji ya ndani akiwa na vilabu hivyo.
Pia ni mshindi mara tano wa UEFA Champions League; mara nne na Real Madrid na moja na Manchester United.
Kando, aliiongoza Ureno kutwaa taji la UEFA EURO 2016. Ana mkataba na Al-Nassr hadi 2025.
Lionel Messi anashika nafasi ya pili kwa kulipwa pesa nyingi zaidi. Messi anaingiza dola milioni 130.
Supastaa wa Argentina anayekipiga Paris Saint-Germain (PSG) Lionel Messi alipata dola milioni 130 na alikuwa wa pili kwenye orodha hiyo.
Messi, 35, alikuwa mshambuliaji wa muda mrefu wa Barcelona hadi alipohamia PSG mnamo mwaka 2021.
Mnamo Desemba, Messi aliiongoza Argentina kutwaa taji la Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar, ikiwa ni ushindi wake wa kwanza wa Kombe la Dunia tangu 1986.
Messi alishinda mataji manne ya UEFA Champions League na 10 ya La Liga ya Uhispania akiwa na Barcelona, na alitwaa taji la Ligue 1 ya Ufaransa katika msimu wake wa kwanza akiwa na PSG.
Mchezaji mwenzake Messi katika PSG, Kylian Mbappe, anashika nafasi ya tatu akiwa na dola milioni 120.
fowadi huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24, alikuwa wa tatu kwenye orodha hiyo, akipata $120 milioni.
Mmoja wa washambuliaji mashuhuri, Mbappe alishinda mataji ya Ufaransa akiwa na PSG na Monaco, na alishinda Kombe la Dunia la 2018 akiwa na Ufaransa.