Timu ya taifa ya soka ya Comoros maarufu Les Coelacantes wataanza mechi zao za kufuzu Kombe la Dunia 2026 mwezi huu wa Novemba dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya kati na Ghana.
Wanavisiwa watafungua safari yao wakiwa chini ya kocha mpya, mwitaliano Stefano cusin (54), kocha wa zamani wa Sudan Kusini, aliyeteuliwa kuinoa Comoros mapema mwezi Oktoba 2, huku akichukua nafasi ya Younes Zerdouk wa Ufaransa na Morocco.
Kwa mujibu wa FIFA, Comoros itapiga mechi yake ya kwanza nyumbani katika mechi ya siku ya pili ya michuano ya kufuzu Kombe la dunia Jumanne, Novemba 21, 2023 katika uwanja wa Moroni- uwanja wa matumizi mengi huko Comoros ambao kwa sasa unatumiwa zaidi kwa mashindano ya riadha.
Mara ya mwisho timu hizo mbili zilipokutana katika kombe la mataifa ya Afrika 2021 Nchini Cameroon, Comoros iliipiga Ghana 3-2 katika mechi ya Kundi C.
Mnamo 2022, timu ya taifa ya kandanda ya Comoro, iliwashangaza wengi kwa kutekeleza mojawapo ya mapinduzi makubwa katika historia ya michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika AFCON, walipoipeleka Ghana nyumbani kutoka AFCON 2021 baada ya kusababisha ushindi usiotabirika wa 3-2 ugenini.
Mwamuzi kutoka Mauritania Bouh Abdel Aziz ndiye ameteuliwa kusimamia mechi ya kufuzu kombe la Dunia la FIFA kati ya Comoro na Ghana.
Comoros iko kwemye kundi I pamoja na Mali, Ghana, Madagascar, Chad na Jamhuri ya Afrika ya kati CAR kwenye mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026.