Argentina nambari moja duniani, Morocco waongoza Afrika huku FIFA ikitoa orodha ya mataifa bora

Argentina nambari moja duniani, Morocco waongoza Afrika huku FIFA ikitoa orodha ya mataifa bora

FIFA imeiorodhesha Tanzania nambari 122 nyuma ya Uganda na Kenya licha ya kuwa timu pekee kutoka Afrika Mashariki kufuzu Afcon 2023.
Lionel Messi wa Argentina akisherehekea kushinda Kombe la Dunia, Lusail, Qatar - Desemba 18, 2022 / Picha: Reuters

Shirikisho la Soka Ulimwenguni, FIFA, siku ya Alhamisi limechapisha rasmi viwango vyake vya robo mwaka huku baadhi ya timu zikipiga hatua kadhaa za kufurahisha kwenye viwango vya ulimwengu.

Timu ya Taifa ya Soka ya Argentina imetambulika kwa mwanzo wake wa kuvutia kwenye ngarambe za kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026 na kuongoza kiwango cha ubora wa Ulimwengu wa soka wa FIFA/Coca-Cola.

Wakati huo huo, nafasi ya pili imechukuliwa na Ufaransa, Brazil imesalia katika nafasi ya (3) ikifuatiwa na England ya (4) na Ubelgiji ya (5) huku timu hizo zikihifadhi nafasi zao katika timu tano za juu ikiwa sawa na orodha iliyotolewa Julai 2023.

Morocco imechupa nafasi mbili juu hadi nafasi ya 13, na kudumisha nafasi yake ya kuwa taifa bora zaidi Afrika. Hata hivyo, Sadio Mane na Senegal ambao ndio mabingwa wa dunia, wamezama nafasi mbili kutoka nafasi ya 18 hadi nafasi ya 20 na kusalia kati ya timu 20 bora ulimwenguni.

DR Congo ndio timu bora zaidi Afrika Mashariki ikifuatiwa na Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Sudan Kusini, Djibouti na Somalia.

TRT Afrika