Carlo Ancelotti, kocha wa Real Madrid / Picha: Reuters

Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amerefusha mkataba wake na Real Madrid hadi juni 2026 Ijumaa kumaanisha kuwa hatakuwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil.

Mnamo Julai mwaka huu, taarifa zilidai kuwa Ancelotti, kocha matata mwenye umri wa miaka 64, angekuwa kocha wa kwanza wa kigeni kuinoa Brazil baada ya takriban miaka 60 pindi tu mkataba wake wa sasa utakapokamilika.

Aidha, matarajio hayo ya Brazil yameifanya Shirikisho la Soka nchini Brazil kumteua Fernando Diniz kuwa meneja wa mpito kabla kwani ilitarajia kumkabidhi Ancelotti kuchukua udhibiti wa Copa America ya 2024.

Huenda hatua ya Ancelloti ni yenye busara kwani, ikilinganishwa na Brazil, matokeo ya Real msimu huu yamekuwa mazuri sana huku wakiwa juu ya La Liga na hata kufuzu raundi ya mtoano ya ligi ya mabingwa ikisajili ushindi sita katika mechi sita.

Ancelloti ni kocha anayesifika sana kwani ameshinda Ligi ya Mabingwa Champions League mara nne, ikiwemo mara mbili na AC Milan ya Italia na mara mbili na Real Madrid.

Vile vile, ameshinda mataji ya ligi kuu katika mataifa mbalimbali ikiwemo na Real na Milan, Chelsea nchini England, Bayern Munich Ujerumani na Paris Saint-Germain Ufaransa.

AFP