Riyad Mahrez wa Algeria apokea tuzo Ya Afcon kutoka kwa rais wa zamani wa CAF Ahmad Ahmad / Picha: Reuters

Serikali ya Algeria kupitia Wizara ya Vijana na michezo imefanya uamuzi huo "ili kuunga mkono watu wa Palestina wenye ujasiri "na kwa heshima ya waathirika katika ukanda wa Gaza," Kituo cha Habari cha Kitaifa cha ENTV kiliripoti.

Aidha, Shirikisho la Soka la Algeria (FAF) pia lilitangaza kusitisha mechi zote, "hadi itakapotangazwa tena" ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono madhila wanayopitia Wapalestina kutokana na mashambulizi ya Israel.

Wakati huo huo, Algeria, ambayo kijadi ni muungaji mkono thabiti wa juhudi za Palestina, ilitangaza kuwa ilikuwa tayari kuandaa "mechi zote rasmi na zisizo rasmi za timu ya taifa ya soka ya Palestina kama sehemu ya maandalizi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 na Kombe la Asia la 2027 ikiwemo kulipia gharama zote zinazohusiana na michuano hiyo.

"Shirikisho la Soka la Algeria, kwa mujibu wa maagizo ya mamlaka kuu ya nchi hiyo na kufuatia ombi lililotolewa na rais wa Shirikisho la Soka la Palestina, Jibril Rajoub, imeamua kuandaa mechi zote rasmi na zisizo rasmi nchini Algeria kama sehemu ya maandalizi ya kufuzu Kwa Kombe la Dunia la 2026 na Kombe la Asia la 2027 ikiwemo kulipia gharama zote zinazohusiana na michuano hiyo," taarifa iliyotolewa na shirikisho hili ilisema.

TRT Afrika na mashirika ya habari