Klabu ya ligi kuu ya soka nchini Ujerumani Mainz imesema kuwa imekatisha mkataba wake na mshambulizi Anwar El Ghazi kufuatia machapisho yake kwenye mtandao wa kijamii kuhusiana na mashambulio ya Israel hukoGaza, licha ya nyote huyo kuufuta tangu wakati huo.
Mainz 05 ambayo iko chini kwenye jedwali ya ligi kuu ya Bundesliga, ilimsaini El Ghazi Septemba mwaka huu.
Mholanzi huyo alisimamishwa kazi mwezi Oktoba kufuatia matamshi yake ya awali kuhusu mzozo huo lakini alisamehewa kurejea mazoezini Jumatatu baada ya kuonyesha majuto, klabu hiyo ilisema.
"FSV Mainz 05 imemaliza mkataba wake na Anwar El Ghazi. Klabu imechukua hatua hii kujibu maoni na machapisho kutoka kwa mchezaji kwenye mitandao ya kijamii," Mainz 05 ilisema katika taarifa.
Jibu la El Ghazi
El Ghazi alijibu kuwa, "kupoteza riziki yake sio kitu ikilinganishwa na dhulma dhidi ya watu wasio na hatia na walio hatarini huko Gaza," El Ghazi aliandika mtandaoni.
Hata Hivyo, El Ghazi, mwenye umri wa miaka 28, alichapisha taarifa mpya Jumatano, huku klabu ya Ujerumani ikisema "haieleweki" na kwamba watachunguza fikira ikiwa watafuata hatua za kisheria.
"Mimi ninapinga vita na vurugu. Ninapinga mauaji ya raia wote wasio na hatia. Mimi siungi mkono aina zote za ubaguzi. Mimi ninapinga 'chuki dhidi ya Uislamu'. Mimi ninapinga chuki dhidi ya Wayahudi. Ninapinga mauaji ya kimbari. Ninapinga ubaguzi wa rangi. Ninapinga ukandamizaji." El Ghazi aliandika
El Ghazi mwenye umri wa miaka 28, aliwahi kuziwakilisha PSV Eindhoven, Aston Villa Na Everton, na amecheza FSV Mainz 05 mechi tatu tu kwa timu hiyo.