Nyota wa Liverpool Mo Salah akata kimya kuhusu hali ya Gaza. Picha : Reuters

Nyota maarufu wa soka wa Misri Mohamed Salah amewataka viongozi wa dunia kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia " mara moja " katika Ukanda wa gaza uliokumbwa na vita.

"Si rahisi kila wakati kuzungumza katika nyakati kama hizi. Kumekuwa na vurugu nyingi na ukatili mwingi mno wenye kuvunja moyo. Maisha yote ni matakatifu na lazima yalindwe," Salah alisema katika video iliyochapishwa kwenye akaunti yake ya mtandao wa X Jumatano.

"Kilicho wazi sasa ni kwamba misaada ya kibinadamu kwa Gaza lazima iruhusiwe mara moja. Watu wa huko wako katika hali mbaya, " Salah alisema katika ujumbe wa video uliochapishwa kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

"Matukio katika hospitali jana usiku (Jumanne) yalikuwa ya kutisha," mshambuliaji huyo wa Liverpool alisema akimaanisha shambulio la anga la Israeli Jumanne kwenye hospitali ya Baptist ya Al-Ahli eneo la Gaza.

"Kilicho wazi sasa ni kwamba, ni lazima misaada ya kibanadamu kwa Gaza iruhusiwe mara moja. Watu wako katika hali mbaya. Natoa wito kwa viongozi wa dunia kuungana ili kuzuia mauaji zaidi ya watu wasio na hatia," Salah alisisitiza.

Salah amekuwa mchezaji wa kutegemewa wa Liverpool tangu 2017 huku akiisaidia timu hiyo kushinda taji la ligi kuu ya Uingereza mnamo 2020 na kufunga mabao 192 katika mechi 315 kwa miamba hao wa Uingereza.

AA