Rui Vitória na wakufunzi wenzake wa kimkakati  walitimuliwa baada ya Misri kutolewa katika hatua ya 16 bora. / Picha: Reuters

Rui Vitoria ametimuliwa kama kocha mkuu wa Misri baada ya miamba hao wa soka barani Afrika kuvunjiwa matumaini ya kunyakua rekodi ya kuwania ubingwa wa nane wa Kombe la Mataifa ya Afrika wiki iliyopita, Shirikisho la Soka la Misri (EFA) lilitangaza.

Katika taarifa, bodi ya wakurugenzi ya EFA "ilimshukuru meneja huyo kutooka Ureno Rui Vitoria na wafanyakazi wake," na kuongeza kuwa "inakagua wasifu wa makocha wa kigeni".

Kwa muda, mkufunzi wa zamani wa al-Ahly, Mohamed Youssef atachukua jukumu la kuinoa timu ya taifa, ambayo ilitupwa nje ya mashindano wiki iliyopita katika mikwaju ya penalti dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kupoteza katika hatua ya 16 bora ilikuwa kidonge chungu kwa Wamisri, ambao walikuwa wamekwenda Côte d'Ivoire wakitumai kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu 2010, mwaka mmoja kabla ya nyota Mohamed Salah kucheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa.

Utendaji duni

Timu hiyo tayari ilikuwa imempoteza nyota huyo wa Liverpool kutokana na jeraha la msuli wa paja, baada ya kile wadadisi wa huko walichokiita kutokuwa na matokeo mazuri katika hatua ya makundi kwa sare tatu.

EFA wiki jana "iliomba radhi" kwa mashabiki wa Misri kwa "kutofikia malengo yao".

Vitoria, ambaye enzi yake na Mafarao ilidumu chini ya miaka miwili, ni miongoni mwa makocha wengi wa AFCON wakiwa njiani kuondoka.

Mashindano hayo yamekuwa ya mafanikio kwa timu zilizotazamiwa kuni dhaifu katika bara hili, na kuwakatisha tamaa vigogo wake.

Mataifa matano ya Afrika yaliyoorodheshwa juu yote yalitolewa kabla ya robo-fainali, pamoja na timu nne zilizofuzu nusu fainali kutoka toleo la mwisho.

TRT Afrika