Kwa mashabiki wa soka Afrika Mashariki, kuna tofauti ya saa tatu kwenye majira kwani Afrika Mashariki wako mbele kwa saa.

Baada ya miaka 40, Baada Ya makala 20 Ya Afcon, hatimaye macho na masikio yote yatahamia Afrika Ya Magharibi tangu nchi hiyo kuandaa kwa mara ya kwanza Michuano hayo hwaka 1984, ambapo timu ya taifa ya Cameroon, maarufu kama Simba Wasiofugika waliibuka washindi.

Kwa jumla, maandalizi ya tukio hili kubwa yamekwisha kamilika, ambapo viwanja sita vitawaka moto pale nchi 26 zitakapotunishiana misuli katika siku 52 . swali linatotawalavVichwa kwa sasa, ni kwa nini hasa michuano hii iitwe Afcon 2023 wakati inafanyika 2024?

Jibu ni rahisi.

Awali, AFCON ilikuwa ifanyike kati ya mwezi wa sita na saba mwaka jana. Hata hivyo hilo halikufanyika kutokana na mvua kubwa zilizoshuhudiwa katika kipindi hicho.

Hatua hiyo ilitoa sababu kwa waandalizi kisogeza mbele michuano hiyo hadi Januri mwaka huu.

Miongoni mwa miji mitano itakayoandaa mechi hizo ni pamoja na Abidjan, mji wa kati wa Bouake, mji wa Kaskazini wa Korhogo, bandari ya kusini Magharibi ya San Pedro na mji mkuu Yamoussoukro.

Viwanja vitakavyotumika ni pamoja na viwanja vitatu vilivyojengwa hivi karibuni vya Korhogo, San Pedro na Yamoussoukro.

Uwanja wa Alassane Ouattara mjini Abidjan, ndio uwanja mkubwa zaidi n autaandaa mechi ya ufunguzi, na mechi ya fainali.

Akwaba ndicho kigaragosi rasmi kitakachotumika kwenye fainali hizo kutoka lugha ya Baoulé Kumanisha Karibu Wakati “Pokou” Ndilo Gozi Rasmi Litakalotumika Kwenye Michuano Hiyo Itakayodumu Kwa Mwezi Mmoja

Mpira huo umepewa jina hilo kwa heshima ya nyota wa zamani wa nchi hiyo, Laurent Ndri Pokou ambaye anatajwa kama baba wa soka la Ivory Coast. Mechi za hatua za kwanza na pili zitaanza Jumamosi, Januari 27, baada ya vipute vya hatua ya makundi kumalizika tarehe 24 Januari.

Itafuatiwa na hatua ya robo fainali, kipute kitakachopigwa Ijumaa Februari 2 na nusu fainali itakayopigwa Jumatano, Februari 7. Mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu itapigwa Jumamosi , Februari 10, na siku ya kumtuza mwali uwanjani ni Jumapili, Februari 11, katika uwanja wa Alassane Ouattara, mjini Abidjan.

Kwa mashabiki wa soka Afrika Mashariki, kuna tofauti ya saa tatu kwenye majira kwani Afrika Mashariki wako mbele kwa saa.

Bingwa wa michuano hii atazawadiwa kitita cha dola za Kimarekani Milioni 7, tofauti na Afcon iliyofanyika Cameroon 2021, ambapo Senegal, maarufu kama Simba Wa Teranga waliweka mfukoni dola za Kimarekani Milioni 5. Je, uko tayaru kuwa Sehemu ya uhondo huu kwa mwezi mzima?

Je, ni kweli kuwa Ivory Coast italibakisha kombe hilo kwenye ardhi yake baada ya kufanya hivyo mwaka 1992 na 2015? kwa sasa nchi hiyo imetenga dola Bilioni 1.5 kujaribu kuhakikisha kombe linachezwa vila wasiwasi.

Inakadiriwa Kuwa takriban mashabiki milioni 1.5 Kutoka pembe zote za Afrika watatua Ivory Coast kuzipa hamasa timu zao.

TRT Afrika