Mashabiki wa Ivory Coast wakiwa kwenye picha ya kujiandaa na mechi ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) 2024 kati ya Côte d'Ivoire na Nigeria. / Picha: AFP

Na Firmain Eric Mbadinga

Kikombe cha furaha cha Modeste Codjo Bessanh kinafurika. Na sio tu kwa sababu nchi yake asili Côte d'Ivoire ilishinda toleo la 34 lililomalizika hivi punde la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Nigeria kwenye fainali.

Katika mchuano wa kusisimua ambao ulishuhudia timu kadhaa za juu zikishindwa na walio chini kufanya vyema, mchezaji thabiti zaidi alikuwa nje ya uwanja.

Biashara ya kukodisha magari ya Bessanh katika kitovu cha uchumi cha Côte d'Ivoire, Abidjan, ilikuwa mojawapo.

Kuanzia Januari 13 hadi Februari 11, AFCON ilikuwa fursa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kupata manufaa ya mvuto wa ulimwengu wa soka na maslahi yanayotokana na michuano hiyo maarufu na inayosubiriwa katika bara hili.

"AFCON ilikuwa tamasha! Ninaamini Côte d'Ivoire inaweza kuandaa Kombe la Dunia," Bessanh aliiambia TRT Afrika. "Wakala wangu ulifanikiwa kukodisha karibu magari yetu yote kwa waandishi wa habari wengi waliomiminika nchini kwa muda wote wa tukio. Binafsi, kila kitu kilikwenda sawa."

Bessanh, ambaye anamiliki takriban SUV na saluni kumi, anakadiriwa kupata kati ya CFA 40,000-100,000 kwa siku kama kodi ya kila gari.

Biashara zilifanya vyema katika miji mingine minne iliyoandaa mashindano hayo pamoja na Abidjan.

Mashabiki wakishangilia ushindi wa Côte d'Ivoire katika Kombe la Mataifa ya Afrika 2024, wakati wa gwaride mjini Abidjan

Pendekezo la muda mrefu

Dk Al Kitenge, mwanamkakati wa kiuchumi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, anasema athari kama vile AFCON inaweza kuwa na uchumi wa ndani haipaswi kupimwa tu kwa faida ya haraka.

"Nchi inapoomba haki ya kuandaa hafla kubwa ya kimataifa, michezo au vinginevyo, ni juhudi za kimahesabu ambazo zinahusisha shughuli za ajabu nyuma ya pazia zenye athari za muda mrefu za kiuchumi," anafafanua.

"Kuna mtiririko wa kifedha unaokuja na vibali, umiliki wa vyumba na migahawa, na mabadiliko mengine. Hii inahusishwa moja kwa moja na mahitaji kutoka kwa miundo hii mikubwa kwa wazalishaji wadogo na wasambazaji. Kwa hivyo, tunaweza kuona kwamba inaingia kwenye mizizi."

Matukio makuu kama vile AFCON pia huanzisha sheria ya ugavi na mahitaji, hivyo kusababisha manufaa kwa soko la bidhaa na huduma katika nchi mwenyeji, bila kujali kama matukio hayo ni ya kimichezo, kiuchumi au kiutamaduni.

Mashabiki wanasherehekea Côte d'Ivoire kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) la 2024, katika wilaya maarufu ya Treiville, mjini Abidjan.

Raha ya ladha asilia

Huko Anoumabo, mojawapo ya wilaya maarufu zaidi za Abidjan, Iliasse Dayamba alichukua fursa hiyo kutoa huduma zake za upishi kwa maelfu ya watazamaji waliokuwa wamekusanyika nchini Côte d’Ivoire kwa ajili ya AFCON 2023.

Dayamba aligundua wakati wa mchuano huo kwamba kushuka na mapato yaliyopatikana katika mgahawa wake, Au Burkina 3, yalitegemea uwepo na uchezaji wa timu mahususi. Biashara iliongezeka mara kwa mara wakati "Mastallion" wa Burkina Faso na "Tembo" wa Côte d'Ivoire walipokuwa wakicheza.

"Tulikuwa na wateja kutoka nchi kadhaa. Wana Ivory Coast walikuwa kundi kubwa zaidi, lakini pia kulikuwa na mashabiki kutoka nchi nyingine. Siku za mechi, mapato yangu yangekuwa ya juu zaidi, hasa kupitia uuzaji wa vinywaji," anaiambia TRT Afrika.

Kama mjasiriamali yeyote anayefanya biashara, Dayamba alijua alihitaji kutumia vyema frusa hiyo.

"Katika hali hii, jambo muhimu zaidi la kufanya ni kukuza bidhaa na huduma za ndani. Unahitaji kuzingatia masoko ya mkoa ili watu waweze kugundua thamani ya mali," anasema.

Kando na uanzishwaji wa sekta ya huduma kama zile zinazoendeshwa na Bessanh na Dayamba, AFCON 2023 ilitoa fursa kwa biashara mbalimbali - kutoka kwa maduka ya vyakula hadi vifaa - katika maeneo ya biashara ya muda karibu na viwanja vinavyoitwa "Villages de la CAN".

Serikali ya Côte d'Ivoire inakadiriwa kuwekeza dola za Marekani 1.5 katika kuandaa toleo la 34 la AFCON, ikitumia sehemu kubwa ya fedha hizo katika ujenzi wa miundombinu, ikiwa ni pamoja na kujenga au kukarabati viwanja sita vya soka.

Mashabiki wa nyumbani wakati wa gwaride mjini Abidjan, Februari 12, 2024.

Kuwekeza kwa siku zijazo

Kwa hivyo, je, miundombinu iliyojengwa kwa hafla maalum hutoa faida kwa kiwango sawa mara tu itakapomalizika?

Dk Kitenge anaamini kila nchi inafanya kazi yake ya nyumbani katika kubadilisha uwekezaji huo kuwa miundombinu yenye faida baada ya kufikia lengo la haraka la kuandaa hafla fulani kwa njia bora zaidi.

"Kwa mfano, ukiangalia Kijiji cha Olimpiki kilichojengwa London mwaka 2012, kila kitu kiliuzwa tena baadaye. Walijenga viwanja mahsusi kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki, lakini kwa namna ambayo vingeweza kuvunjwa baadaye ili kutumwa tena kwa kiwango kidogo, " anaiambia TRT Afrika.

"Unapounda miundombinu kwa madhumuni ya muda mfupi, lazima uwe na mpango wa matumizi baada ya tukio. Na hiyo inategemea uwezo wa kila nchi kujipanga upya."

TRT Afrika