Tabia za ubaguzi miongoni mwa watu wa Morocco na Algeria licha ya kuwa na historia moja

Tabia za ubaguzi miongoni mwa watu wa Morocco na Algeria licha ya kuwa na historia moja

Mataifa ya Morocco na Algeria yana mfanano mkubwa hasa wa kidesturi lakini pia tabia za kuwarudisha nyuma vilevile ni sawia miongoni mwa watu wa mataifa hayo; kiasi kwamba utofauti wao ni kiwango cha tabia hizo na wala sio wa kiasili.

Msemo maarufu wa Descartes kuwa –“Akili ya kawaida ndiyo yenge mgao sawia ulimwenguni” hauingii akilini unapodadisi tabia za baadhi ya watu wa Morocco na Algeria katika nyakati za sasa. Tabia za ubishi na ubaguzi miongoni mwao zimetawala pakubwa; mara ubishi juu ya chakula aina ya couscous, mavazi ya kaftan na vigae vya ujenzi au hata watu tajika katika historia yao ya pamoja kama vile; Tarik Ibn Ziyad, Almohades na Ibn Batouta.

Morocco na Algeria ni mataifa yaliyo na mfanano mkubwa; sema wa kifamilia, mila, desturi, lugha n ahata lafudhi lakini watoa-maoni wakubwa na muhimu wametawaliwa na mada nyepesi zisizo na tija. Kwa mfano utashangaa kuwaona raia wa Morocco wakikerwa na mifumo/michoro ya vigae iliyoko kwenye jezi za timu ya taifa ya Algeria.

Kwengineko utakuta meneja wa shirika la ndege Algeria kasimamishwa kazi eti kwa kuwa amesambaza vipeperushi vinavyoonesha usanifu wa majengo ya Morocco. Kuna uelewa tatanishi sana wa historia miongoni mwao.

Utata mara nyingi pia huchochewa na ukweli kwamba neno “Maghreb” kwa Kiarabu lina maana ya ‘Maghreb’ na ‘Morocco.’ Hivyo basi ‘Bab al Maghariba,’ ambao ni mlango wa Msikiti wa Al Aqsa humaanisha ‘Mwafrika kutokea Afrika ya Kaskazini’ na ‘raia wa Morocco’ kwa Kiarabu.

Kwa hakika Morocco sio Algeria; na wala Algeria sio Morocco lakini ukweli kuwa mataifa hayo mawili yana mfanano mkubwa wa historia hauwezi kupuuzika.

Siku moja kamanda wa mahakama ya kifalme ya Morocco aliwahi kunikuta nikitazama ‘Qubbat Annasr,’ ambayo ni nembo ya Uhuru wa Morocco – kwa maana kwamba sehemu maalum ya kufanyia maaamuzi na sherehe muhimu. “Nyenzo iliyotumika katika nembo hii inatoka wapi?” kamanda aliniuliza. Nikamjibu kwa haraka “inatoka Tetouan kwani ni tofauti ya mtindo wa Fez.”

“La umekosa,” alinieleza Kamanda, “Hii ni ya kutoka Tlemcen,” na kuongeza kuwa aliyeileta kutoka Tlemcen alikuwa ni Fqih Al Maamri karne iliyopita. Fqih Al Maamri aitokea Kabylie nchini Algeria na alikuwa na cheo cha Mkurugenzi wa Baraza la Mawaziri na mwalimu wa Binti ya Mfalme.

Pindi baada ya Morocco kujinyakulia uhuru wake aliteuliwa Waziri Mkuu wa Nyumba ya Kifalme. Huenda ikawashangaza watu wengi wa Morocco kugundua kuwa waziri mkuu wa nyumba ya kifalme alkuwa ni wa kutoka Algeria na kwamba Mkuu wa Itifaki Kaddour Benghabrit alikuwa ni mzaliwa wa Tlemcen.

Aidha Rais wa kwanza wa Algeria baada ya Uhuru Ahmed Ben Bella alikuwa na asili ya Morocco kutoka Marrakch. Orodjha ya viongozi hawa kutoka mataifa haya mawili ni kubwa na utagundua kuwa ni mataifa yaliyo na utofauti finyu sana na mfanano mkubwa wa historia.

Utagundua Mmorroco kutoka Rif ana mfanano mkubwa na Mkabyle kuliko hata mwenzake kutoka Marakkech. Aidha Mfassi vilevile anakaribiana zaidi na mtu kutoka Tlemcen kuliko mwenzake wa Atlas. Kwa hivyo basi kuwaangalia watu wa mataifa haya mawili kama tofauti ni Jamabo la ajabu sana. Sio rahisi. Ni nchi mbili zilizo na uwiano mkubwa.

Yawezekana sasa mzozo huu uliochochochewa na jezi za timu ya taifa ya Algeria utawakumbusha watu wa Morocco na Algeria kuwa ni wamoja na historia yao ina uwiani mkubwa na kwamba wana hatima moja.

TRT Français