Kwa nini uhusiano kati ya Macron na Morocco umezorota zaidi?

Kwa nini uhusiano kati ya Macron na Morocco umezorota zaidi?

Ushawishi wa Ufaransa katika makoloni yake ya zamani barani Afrika unapungua. Uhusiano wake na Mali umevunjika huku ule wa Burkina Faso unayumba. Lakini je, Macron anaweza kumudu kuupoteza uhusiano na Morocco?

Na Martin Jay

Hivi majuzi tu iliripotiwa kwamba vikosi mamluki vya Wagner vilikuwa vikitumwa kufanya kazi za Serikali ya Burkina Faso, mshirika wa Kifaransa huko Afrika Magharibi ambayo mara chache hujitokeza katika vyombo vya habari, hasa vinavyutumia lugha ya Kiingereza. Hili limeanza kuzitia hofu nchi za Magharibi, bila kusahau Serikali ya Ghana ambayo inawaona wanamgambo hao kama tishio lijalo. London na Washington zinaona kwamba Ufaransa inapoteza ushawishi wake katika makoloni yake ya zamani na kwamba - kiuhalisia - Urusi itachukua nafasi yake kama mtawala mpya.

Wana haki ya kuwa na wasiwasi. Hii tayari inatokea, ingawa taratibu, kufuatia hatua hio ya Mali, na kwa upande mwingine Burkina Faso kuanza kutegemea msaada wa Urusi. Macho yote sasa yapo kwenye nchi hii ya Afrika magharibi kuona kama itaenda mbali zaidi kwa kuvunja uhusiano na Elysee, ingawa wengi wanaona kwamba ingawa hii haijafanyika rasmi, kwa namna nyingine, tayari hatua hii imefikiwa. Burkina Faso imefuata utaratibu uliotumika na jirani yake Mali ambayo utawala wake wa kijeshi ulipambana na Macron tangu siku ya kwanza. Vyombo vya habari vya Ufaransa vilipigwa marufuku kwa kuripoti juu ya upinzani (kila mara huitwa 'magaidi' na serikali za Kijeshi), ikifuatiwa na kufukuzwa kwa jeshi la Ufaransa.

Kwa upande wa Mali, kwanza ilikuwa ni wanajeshi wa Ufaransa, kisha vyombo vya habari, halafu mashirika yasio ya kiserikali (NGOs). Kwa upande wa Burkina Faso, mashirika yasiyo ya kiserikali na wanajeshi wa Ufaransa bado wapo kwa idadi ndogo lakini kutokana na hali ya sasa ya utawala wa kijeshi ambao walichukua madaraka miezi kadhaa iliyopita kuamini kuwa Wafaransa wanaunga mkono utawala uliopita, ni suala la muda tu kabla ya watawala hao wa Ouagadougou kufuata mfano wa Mali.

Asilimia 50 ya akiba ya dhahabu kubaki Paris?

Hilo likitokea, basi Burkina Faso itaonyeshwa kwa mara nyingine kwenye CNN na BBC kama hadithi mpya ya kushindwa kwa Afrika kuondoa kasumba ya utawala wa kijeshi baada ya kuuondoa ukoloni. Hata hivyo, koloni hili la zamani la Ufaransa ya Kiafrika liligonga vichwa vya habari hivi majuzi tu baada ya kipande cha video cha Waziri Mkuu mpya wa Italia kiliposambazwa na kudai kwamba ni Wafaransa ambao "walichukua" asilimia 50 ya akiba yake ya dhahabu na, kwa sababu hiyo, walifanywa watumwa na kuwa nchi inayozalisha wahamiaji wanaotafuta hifadhi nchini Italia.

Kwa kweli, hoja za Waziri Mkuu Giorgia Meloni hazikuwa sahihi. Ufaransa haihifadhi dhahabu yoyote ya Burkina Faso, ingawa kwa namna fulani inadhibiti uchumi wake - sawa na nchi nyingi za Afrika Magharibi - kupitia sarafu iliyoanzishwa na Wafaransa, ambayo leo hii, inachukuliwa kwa kiasi kikubwa kama kitanzi cha ukoloni shingoni mwa nchi hizi.

Maneno ya Meloni sio sahihi, lakini hoja yake ni nzuri. Ikiwa nchi hizi zingeweza kujiondoa kwenye pingu za Ufaransa na uhusiano wake wa kikoloni na Elysee, zinaweza kuwa na nafasi nzuri ya kujiendeleza kisiasa na kiuchumi.

Iwapo Burkina Faso itachukua hatua ya kuwatimua wanajeshi wa Ufaransa kutoka nchini mwake na kuangalia zaidi upande wa Urusi ili kupata msaada, basi kuna hatari kubwa kwamba mataifa mengine ya Kiafrika yenye ushirika na Ufaransa kufuata mtindo huo na kupelekea Ufaransa - na nchi zingine za Magharibi - kutupwa nje ya karibu nusu ya Afrika. Mabadiliko hayo yatakuwa ya aina yake inaweza kuonekana kama sehemu ya nadharia ya "mwanzo upya" ambayo sote tunaendelea kusikia. Bila shaka, kutakuwa na washindi na walioshindwa.

Je, nchi za Magharibi zitakubali kushindwa katika kinyang’anyiro hiki?

Nafasi ya Morocco

Hapa ndipo Morocco inapoingia. Hivi majuzi, Macron alimtuma waziri wake huko Rabat kufanya kazi na Wamorocco na kuandaa mazingira kwa ajili ya ziara yake binafsi kwa Mfalme mwezi Januari. Mgogoro kati ya Macron na Morocco, unaweza kutajwa kuwa unatokana na msimamo mkali wa Macron dhidi ya uhamiaji. Lakini kiuhalisia, mgongano unatokana na kushindwa kwa Macron kutoa msimamo thabiti juu ya madai ya Rabat kwa Sahara Magharibi. Vyombo vya habari viliripoti kuwa mahusiano yamerejeshwa wakati Waziri huyo wa Ufaransa na Waziri wa mambo ya nje wa Morocco walipopiga picha wakitabasamu na kutangaza kuwa mambo yalikuwa sawa. Lakini hii sio habari ya kweli.

Ukweli ni kwamba watawala wa Rabat ni wameng’ata meno kichinichini dhidi ya Macron na Ufaransa. Weka pembeni kidogo habari ya Burkina Faso na Mali. Hakuna mtu katika bara zima ambaye amechoshwa na Wafaransa kuliko Wamorocco kwani uhusiano wao maalum na Elysee, mwishowe, haukuwapa chochote isipokuwa kipandauso na majuto ya kudumu.

Wakuu wa Rabat wangependa sana kwenda mfumo wa 'kutofungamana na upande wowote' duniani, iwe Umoja wa Ulaya, Marekani, Urusi au hata mkoloni wake wa zamani, Mfaransa. Ukweli, tofauti na Burkina Faso, ambayo bado inategemea sana misaada ya Ufaransa, Wamorocco wanafahamu fika kiwango cha uwekezaji wa Ufaransa huko Casablanca na kwa hivyo wanafungamana na Paris wapende-wasipende. Uuhusiano huo na makampuni ya Ufaransa nchini Morocco unaweza kuwa ndio kiunganishi pekee ambacho Macron anaweza kuwa nacho ikiwa mambo yataendelea kama awali.

Mkutano na waandishi ukisindikizwa na tabasamu

Katika mkutano na waandishi wa habari huko Rabat, kwa wale wenye na ufahamu wa kutosha wa uchunguzi na itifaki, Bourita alifanya jambo la kushangaza: alitoa hotuba yake katika lugha ya asili ya darija, ikimlazimu mwenyeji wake kutumia mtafsiri. Hii haijawahi kutokea hapo awali na, ikiwa na kinyume na misingi ya kidiplomasia. Tukio hili lilituma ujumbe wenye tafsiri mbili kwa Macron: Muda wako unakaribia kwisha. Tuko tayari kufunga uhusiano wote na Ufaransa ikitulazimu.

Kimsingi, ni uhusiano wa Moroko na Ufaransa ambao unaweza kumuokoa Macron na Mataifa ya Magharibi katika Afrika. Ushawishi wa Morocco katika bara hilo unakua kwa kasi ya kuvutia na umeenea hasa katika makoloni haya ya zamani ya Ufaransa, ambako tayari kuna benki zake huko.

Ukweli ni kwamba karibu ulimwengu wote wa Kiarabu unaelekea kwenye mtindo usiofungamana na upande wowote.

"Ulimwengu wa Kiarabu umegoma kufuata upepo katika mwelekeo wa siasa za za kimataifa ambazo zinasisitiza ushirikiano wa aidha Marekani au China na, kwa kiasi kidogo, Urusi kupitia lenzi ya ushindani wa mataifa hayo yenye nguvu," anaandika Hafed Al-Ghwell.

"Kwa kweli, sehemu kubwa ya kanda ya kiarabu inaendelea na itaendelea kujiweka mbali na mtazamo rahisi kama huu, ya kufadhili kwa kutumia ushindani unaozidi kufuata masilahi yake".

Mtaalamu huyo wa DC angeweza kuzungumza juu ya Ufaransa na Morocco, ambayo kwa hakika inaonyesha majeraha ya ukoloni ambayo huonekana kila mahali nchini Morocco, na kwa upande mwingine kuonyesha Wazungu wananvyolazimishwa kupitia mchakato wa kufedhehesha ili kupata ukaazi -- ikiwa ni malipo ya jinsi watu wa Moroko wanavyotendewa huko Uropa.

Hakuna ubishi kuwa Wamorocco wana uhusiano-tata na Wafaransa, ambao bado wanaamini kuwa ni jukumu lao kukosoa ukiukwaji wa haki za binadamu wa Rabat, mfano kamatakamata ya hivi karibuni ya wale ambao wanaokena ni wakorofi.

Ijapokuwa inafuata mwelekeo wa nchi za GCC kuwa 'hazisizofungamani', Rabat inaweza kupata bahshishi ya pekee ambayo ni kama ndoto kwa Abu Dhabi na Riyadh. Moroko inaweza kuondoa nafasi ya Ufaransa na kukaribisha mshirika mpya kama Ukaya au Markeni kama ambayo Uturuki ina uhuru wa kuamua kati nchi za Magharibi na Urusi.

Wakosoaji wa watawala wa Morocco wanasema Rabat haina rekodi nzuri ya kutumia fursa vizuri. Utawala huo bado una safari ndefu ya kuitwa ‘unaopokea madiliko’. Ni kana kwamba mifumo yote inangojea ikulu kutoa agizo la kuhamia ulimwengu unaozungumza Kiingereza, ambapo, kwa kweli, fursa nyingi za uwekezaji Moroko ziko tayari kutengeneza faida.

Ule mkosi wa kupiga 'hatua mbili mbele, tatu nyuma' ambayo Morocco wakati mwingine inaonekana kuwa mhanga mkubwa - kwa mfano hivi karibuni Moroko ilipata fursa ya Kombe la Dunia, ambalo bahati mbaya pia liligubikwa haraka na kashfa ya rushwa ndani ya bunge la Ulaya. Baa hilo liingefutika kwa Moroko kuchukua jukumu muhimu katika kuziweka nchi hizi za Kiafrika zinazozungumza lugha ya kifaransa kambi ya Magharibi, na kuifanya Moroko kuwa nchi yenye nguvu kubwa ya kikanda ambayo Marekani, Ufaransa na EU zingelazimika kuheshimu.

TRT Afrika