Oxfam inaripoti kwamba wastani wa asilimia 70 ya nguo zinazotolewa duniani kote zinaishia Afrika. / Picha: Reuters

Na

Melody Chironda

Biashara ya ubunifu wa mitindo wa haraka unaongoza kwa kutupa taka za nguo katika nchi zinazoendelea, na kuendeleza uchafuzi na uharibifu wa mazingira na ukosefu wa haki wa kijamii. Na Afrika ndio kitovu cha mzozo huu unaokua kutokana na biashara hiyo.

Bara hili ndilo kivutio cha biashara hii ya ubunifu yenye mamilioni ya tani za nguo na nguo zilizotumika kila mwaka, ambazo nyingi ni za ubora duni na mara nyingi hutumiwa mara moja kwenye maeneo ya kazi na baadae kutupwa

Hii inachafua mazingira, inaleta hatari za kiafya kwa jamii, na kuongeza uchafuzi wa hali ya hewa.

Katika miaka ya hivi karibuni, upande wa biashara ya mitindo umedhihirika, na kufichua athari za kimazingira na kijamii na kiuchumi.

Uchunguzi wa hivi karibuni wa gazeti la kila siku la Aftonbladet umeonyesha kuwa watengenezaji wa mitindo mbalimbali ya nguo wanasafirisha mamilioni ya tani za nguo hadi nchi za Kiafrika, ambako mara nyingi hutupwa au kuchomwa moto.

Haya yanajiri baada ya wanahabari hao kutafutwa na chanzo ambacho hakikutajwa jina lake kikidai kuwa kampuni ya H&M hukusanya nguo zilizokwishatumika lakini mara nyingi huzipeleka katika nchi zinazoendelea ambapo hutupwa kwenye madampo au kuchomwa moto bila udhibiti mzuri wa mazingira.

Viwanja vibaya zaidi vya kutupa taka

Ili kuthibitisha madai hayo, wanahabari hao walificha Apple Airtags (vifaa vidogo vya kufuatilia vyenye umbo la sarafu vilivyoundwa ili kuwasaidia watumiaji kutafuta na kufuatilia mali zao za kibinafsi) kwenye baadhi ya nguo za kampuni ya H&M zilizonunuliwa kwenye duka la mitumba na kuziwasilisha kwa kampuni ya H&M ili kuchakatwa tena.

Nguo hizo zilipaswa kupangwa katika kituo cha uchakataji nje ya Berlin lakini kwa hakika ziliuzwa kwa makampuni ya kibiashara nchini Ujerumani ambayo inatengeneza na kuuza nje na kutumia kama nguo za mitumba. Kisha makampuni hayo hubana nguo hizo ziwe marobota au mafungashio makubwa ili kusafirishwa hadi Afrika Magharibi, ambako ziliuzwa upya, au nyingine hutumika katika Ubunifu na zilizoharibiwa hutupwa kwenye madampo.

Nguo hizo zilifuatiliwa hadi kwenye baadhi ya maeneo mabaya na machafu zaidi ya kutupa taka duniani, na hivyo kusababisha athari mbaya kwa mazingira na uchumi wa nchi za nchi hizo, ilieleza Aftonbladet.

Uchunguzi huo unatia shaka juu ya ahadi ya kampuni ya H&M ya kuongoza kazi zake kuelekea sekta ya urafiki wa mazingira, haki, na usawa wa ubunifu wa mitindo mbalimbali ya mavazi. Kampuni hiyo ilizindua kampeni ya kimataifa ya ukusanyaji wa mavazi mwaka 2013, ikiahidi kukusanya asilimia 95 ya nguo ambazo hutupwa kila mwaka.

Kampuni ya H&M iliahidi kuuza tena nguo ambazo zinaweza kuvaliwa tena, na hii inaashiria mapambano ya sekta ya biashara rejareja ili kukabiliana na mwisho na nguo hizo zilizoisha muda wake.

Katika moja ya majibu yalioandikwa na kampuni ya H&M yaliyojibu madai hayo kwa kusema kwamba "ni kinyume kabisa na nguo hizo kuwa taka". Taarifa hiyo iliongeza,

"Tunajua kuwa bado kuna changamoto zinazohusiana na ukusanyaji na urejeleaji wa nguo, lakini pia tunaona kuwa suluhu kubwa zaidi za kuchakata nguo zinaandaliwa, ambayo ni nzuri sana. Kampuni ya H&M inashughulikia suala hilo kikamilifu na pia Inawekeza katika kutafuta suluhisho.

Uchunguzi huo umeangazia athari mbaya za kimazingira na kijamii na kiuchumi zinazotokana na utupaji wa uchafu wa nguo barani Afrika. Tatizo hili limesababisha uchafuzi wa mazingira, uchafuzi wa maji, matatizo ya afya, kupoteza kazi, na matatizo ya kiuchumi. Je, tunaweza kufanya nini ili kukomesha hili?

Afrika sio dampo

Isaac Kaledzi, ripota wa Deutsche Welle, aliripoti kuwa hali ya sasa ya mazingira ya Afrika inaweza kulizuia bara hilo kufikia malengo yake ya mazingira safi na kulifanya kuwa katika hatari zaidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Oxfam inaripoti kuwa takriban asilimia 70 ya nguo zinazotolewa duniani kote huishia Afrika, huku nyingi zikitupwa kutokana na ubora duni. Wakati wafadhili wengi wanakusudia nguo zao zitumike tena, ukweli ni kwamba nguo nyingi hizi hazifai kwa masoko ya Afrika. Hii inatokana na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na ukweli kwamba nguo nyingi zinazotolewa zimepitwa na wakati, huchakaa au kuharibika.

Sekta ya ubunifu wa mitindo ni mojawapo ya wachafuzi wakubwa wa vyanzo vya maji baridi kutokana na mavazi yaliyotumika ambayo huingia kwenye mifumo ya mito, mara nyingi huishia kwenye bahari, kutoka ambapo inaweza kuoshwa hadi kwenye fukwe, na kuhatarisha viumbe vya baharini na mazingira.

Kulingana na Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa wa Ellen MacArthur, na Biashara ya Hali ya Hewa, sekta ya ubunifu wa mitindo wa mavazi unazalisha asilimia 10 ya hewa chafu ya kaboni duniani - zaidi ya usafiri wa anga na usafiri wa baharini kwa pamoja.

Mara tu baada ya kutupwa kwenye dampo, taka za nguo zinaweza kuchukua mamia ya miaka kuoza. Inaweza pia kuchafua udongo na maji na kuvutia wadudu na panya, ambao wanaweza kueneza magonjwa. Kuchoma taka za nguo hutoa kemikali hatari angani.

Ripoti ya 2017 ya Ellen MacArthur Foundation iligundua kuwa biashara hiyo hutumia karibu asilimia 2.6 ya maji safi ya ulimwengu, ikionyesha athari yake kubwa ya mazingira, Kiasi cha maji ya fulana moja ya pamba ni kama lita 2,700. Uzalishaji wa nguo za mitindo wa haraka pia huleta uchafuzi wa hewa, ambayo inaweza kusababisha matatizo ya kupumua na kuchangia mabadiliko ya hali ya hewa.

Jinsi taka za nguo zinavyoiharibu Afrika

Soko la Kantamanto huko Accra, Ghana, ni kitovu cha nguo zilizotumika kutoka nje ya Afrika Magharibi. Wauzaji wakubwa wa nguo zilizotumika nchini Ghana ni Uingereza, Canada, Marekani, Uholanzi, Uchina, Korea na Australia, kulingana na Eco-age.

Tatizo la upotevu wa nguo haliko nchini Ghana pekee. Nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara zimeathiriwa na janga hili, zikiwemo Nigeria, Zimbabwe, Kenya, Uganda, Tanzania na Zambia.

Soko la Gikomba, kitovu cha nguo za mitumba nchini Kenya, pia linakabiliwa na madhara. Soko limejaa nguo duni ambazo haziwezi kuuzwa. Nguo hizi huishia kwenye lundo, mito, na maeneo ya kutupa, na kuchafua mazingira. Biashara ya nguo za mitumba imehusishwa na unyonyaji wa vibarua, kwani baadhi ya wafanyakazi wanaochambua na kuchakata nguo zilizotumika wanalipwa mishahara ya umaskini na kufanya kazi katika mazingira duni.

Wengine wanaweza kusema kuwa kufurika kwa biashara za bei nafuu, za mitumba kumetoa nguo za bei nafuu kwa mamilioni, lakini pia kumesababisha upotevu wa kazi katika biashara ya nguo na nchini humo. Viwanda vingi vya ndani vimelazimika kufungwa na kusababisha upotevu wa ajira na kudorora kwa viwanda hivyo kusababisha matatizo ya kiuchumi.

Uwanja wa kutupa taka kwa Ulaya

Tatizo la Afrika kama dampo la Ulaya ni kubwa sana, lakini haliwezi kuzuilika.

Tofauti kati ya juhudi za uendelevu kati ya Global North na Global South ni suala kuu na kubwa linalohitaji kushughulikiwa. Bidhaa za mitindo ya nguo ya haraka, haswa, zimekosolewa kwa kutanguliza uwajibikaji wa mazingira katika soko lao la nyumbani huku zikipuuza matokeo katika mataifa yanayoendelea.

Tofauti hii inadhihirika katika nchi za Kiafrika, ambapo chapa mbalimbali za mitindo ya nguo hupata nyenzo kutoka kwa nchi zinazoendelea zilizo na kanuni kali za mazingira, hutengeneza nguo kwa kutumia kemikali hatari na rangi, na kusafirisha nguo kwa umbali mrefu, ambayo huchangia mabadiliko ya hali ya hewa.

Katika Global North, chapa za mitindo ya nguo za haraka zinazidi kufuata mazoea endelevu, kama vile kutumia nyenzo zilizosindikwa na kupunguza matumizi ya maji. Hata hivyo, katika Ulimwengu wa Kusini, ambapo chapa hizi hupata nyenzo zao na kuzalisha nguo zao kwa ajili ya matumizi ya Baadae.

Biashara ya nguo za mitumba ni moja kati ya nguzo kubwa ya kiuchumi barani Afrika, lakini pia ina matokeo mabaya. Ili kupunguza athari hizi mbaya, baadhi ya nchi za Afrika zimetekeleza sera za kulinda viwanda vyao vya ndani vya nguo.

Kwa mfano, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imeunda misamaha au viwango maalum vya ushuru ili kulinda viwanda vya ndani. Hata hivyo, sera hizi pia zinaweza kuwa na matokeo yasiyotarajiwa, kama vile kuzuia ufikiaji wa nguo za bei nafuu kwa watumiaji wa kipato cha chini.

Katika Afrika Mashariki, nchi kama Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, na Burundi zote ziliratibiwa kusitisha biashara ya nguo za mitumba ifikapo 2019, UN yaripoti. Hata hivyo, ni Rwanda pekee iliyotekeleza mpango huu.

Nchi nyingine zimechagua kutofanya hivyo, zikitaja faida za kiuchumi za biashara ya nguo za mitumba. Nchi nyingi za Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa zina wasiwasi kwamba ikiwa zitakomesha biashaŕa ya nguo za mitumba, zitapoteza kazi na mapato ambayo biashaŕa hiyo inazalisha. Nigeria imejaribu kujilinda kwa kutoruhusu uingizaji wa nguo za mitumba. Lakini marufuku hiyo inadhoofishwa na ulanguzi kutoka nchi jirani - kama vile Benin.

Hatimaye, mzozo wa taka za nguo barani Afrika hutumika kama simu ya kuamsha kimataifa, na kutuhimiza na kutambua athari za kimazingira na kijamii za mitindo ya haraka.

TRT World