Na Edward Paice
"Hii ni karne ya Afrika," alisema rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, mnamo Septemba 2019. Ikiwa alikuwa anaongelea demografia pekee, madai yake hayangekuwa ya kupingwa.
Uhakika huu unadai kutambuliwa zaidi katika nchi zilizoendelea na inafaa kukubalika zaidi kutoka kwa na serikali za barani Afrika.
Ukweli mpya unapambazuka.
Tangu kupata uhuru, nchi za Afrika zimepitia, kwa maneno ya mtaalamu mmoja wa idadi ya watu, "msukosuko mkubwa zaidi ya idadi ya watu katika historia".
Mnamo mwaka 1950, bara lilikuwa na chini ya asilimia 10 ya idadi ya watu ulimwenguni. Ifikapo mwaka 2050, robo moja ya dunia itakuwa ya waliozaliwa waafrika.
Kinyume chake, idadi ya watu barani Ulaya itakuwa imepungua kutoka asilimia 20 ya jumla hadi chini ya asilimia 10 katika muda huo huo.
Afrika itachangia zaidi ya nusu ya ongezeko la watu duniani katika miongo mitatu ijayo. Ndani ya kizazi, kutakuwa na Wanigeria wengi kuliko Wamarekani, na idadi ya watu wa Afrika Mashariki na Magharibi itakuwa imeongezeka zaidi ya wale wa Ulaya au Amerika ya Kusini.
Kufikia mwisho wa karne hii, waafrika watakuwa asilimia 35-40 ya raia wote ulimwengu.
Huu sio 'mlipuko' wa idadi ya watu, kwani mara nyingi huitwa; badala yake, ni kuongezeka kwa kasi, kwa idadi ya watu.
Afrika itakuwa kigezo kikuu cha wakati ambapo idadi ya watu duniani inafikia kilele - suala la umuhimu wa ishara kwa makadirio ya mabadiliko ya hali ya hewa, usalama wa chakula na mengine mengi zaidi.
Bara changa zaidi
Ni nini kilisababisha ukuzi huo wa haraka na endelevu? Kuna vyanzo viwili:
Mnamo 1950, umri wastani wa kuishi barani Afrika ulikuwa unasemekana kuwa chini ya miaka 40. Leo ni zaidi ya 60 na imetarajiwa kufikia karibu 70 kufikia katikati ya karne.
Wakati huo huo, kiwango cha jumla cha uzazi , idadi ya wastani ya uzazi kwa kila mwanamke - inabakia zaidi ya nne. Bado itakuwa juu zaidi ya tatu mwaka 2050. Kufikia wakati huo, idadi ya watu wa nchi 60 duniani kote itapungua.
Italia na Korea Kusini, kwa mfano - zinaweza kuona idadi yao ikipungua kwa nusu katika karne ya 21 ikiwa watashindwa kuongeza viwango vya uzazi.
Kipengele cha kushangaza zaidi cha kuongezeka kwa idadi barani ni ujana wake. Umri wa wastani wa waafrika mnamo 2020 ulikuwa kati ya miaka 18.6 tu na 24.4 saskazini mwa Afrika, na 17.5 katika eneo la jangwa la Sahara.
Hii ni chini sana hata ya wastani wa miaka 27.9 kwa nchi zilizosemekana kuwa 'chini ya maendeleo' na umoja wa mataifa, kama ilivyo kwa Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara.
Hakuna demografia ya ‘Kiafrika’
Afrika Kusini, Morocco, Libya na Tunisia ziko katika hali ya zaidi ya watoto wawili kuzaliwa kwa kila mwanamke, huku mwanamke wa Nigeria wanapata watoto saba kwa wastani.
Katika sehemu kubwa ya dunia, upatikanaji wa elimu bora kwa wanawake umelinganishwa na uzazi wa watoto wachache. Lakini nchini Nigeria, uzazi kwa wanawake ipo katika wastani wa watoto nne, hata miongoni mwa wanawake ambao wamemaliza elimu ya sekondari.
Miongoni mwa wanawake waliosoma hadi sekondari nchini DRC, ni karibu watoto sita. Nchini Ghana, ambayo inachukuliwa kuwa kiongozi wa bara katika elimu ya sekondari ya wanawake na matumizi ya njia za kisasa za uzazi ipo na wastani wa uzazi wa watoto karibu nne kwa kila mwanamke.
Nchini Malawi pia, matumizi makubwa ya njia za kisasa za uzazi wa mpango bado hazijasababisha kiwango cha uzazi kushuka chini ya watoto nne kwa kila mwanamke.
Wanawake matajiri zaidi, na wale wanaoishi katika miji mikubwa, kwa kawaida wanataka watoto wachache.
Hata hivyo wanawake wa Angola katika nchi tajiri zaidi wana watoto wanne kwa wastani, wale wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo wana karibu sita, na nchini Uganda na Nigeria, karibu wanne.
Jijini Addis Ababa, nchini Ethiopia , wanawake wanaweza kuwa na chini ya watoto wawili kwa wastani, lakini hiyo ni hitilafu ya kihistoria kati ya makaazi ya mijini ya Ethiopia - na katika miji ya Nigeria, kiwango cha uzazi ni watani wa watoto nne .
Afrika Inapanda
Licha ya uzoefu wa karne nyingi na Afrika, nchi zilizondelea hazijui bara hilo vizuri na bado zinaonyesha nia ndogo ya kurekebisha hili.
Hili linahitaji kubadilishwa haraka, na lengo kuu la kuandika kitabu cha “Youthquake” lilikuwa
Afrika itazalisha takribani nusu ya ajira duniani katika miongo ijayo. Idadi kubwa zaidi ya watu, pamoja na maendeleo ya kiuchumi na rasilimali nyingi, itaathiri mifumo ya biashara ya kimataifa.
Ongezeko la idadi ya watu barani Afrika umekuwa msingi muhimu wa kuvutia sera zaidi za kidiplomasia na uwekezaji kutoka nchi zilizoendelea kama Uchina, Uarabuni, Uchina , India na Turkiye .
Afrika itakuwa muhinu sana katika mapambano ya kukomesha ongezeko la joto duniani na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Ushawishi wa Afrika na waafrika kwenye michezo, muziki, mitindo na dini unazidi kuongezeka.
Kwa kifupi, ni maswala machache sana katika miongo ijayo ambayo haitaathiriwa na Afrika , bara lenye idadi kubwa ya watu.
Edward Paice ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Afrika, Africa Research Institute , yenye makao yake makuu London. Kitabu chake kipya zaidi kinaitwa ‘Youthquake - Why African Demography Matters’