Kati ya mfumko wa bei, ukosefu wa ajira, ongezeko la deni la kitaifa, ufisadi ulokithiri, na janga baya la kibinadamu, Changamoto zinazokabili Rais mpya ni nzito.
Kufikia Septemba 13, 2022, William Ruto, akiwa na miaka 55, amekua rasmi Rais wa tano wa jamuhuri ya Kenya toka nchi kupata uhuru mwaka 1963. Alikula kiapo mbele ya mahakama kuu Nairobi, huku mpinzani wake wa karibu Raila Odinga, wa miaka 77, akikosa kuhudhuria, alishindwa kwa kura 233,000 pekee. Naibu Rais alishinda kwa asilimia 50.49 ya kura, ilhali Odinga alipata asilimia 48.85, ikiwa ni mara ya tano kukosa kiti cha urais, licha ya kuungwa mkono na Rais aliyeondoka Uhuru Kenyatta.
Muda unayoyoma na ni dhahiri kwamba William Ruto hana muda mrefu kama alivyodhani, kwa jinsi watu walivyokua na matarajio makubwa ukilinganisha na changamoto za uchumi na hali nzito za kibinadamu.
Hali tayari ni nzito nchini Kenya kwa shida ya mfumko wa bei ambao umefikia asilimia 8.3 kufikia Agosti, dhidi ya asilimia 7.5 mwaka 2021, japo lengo lilikuwa kupunguza hadi asilimia 5.5 mwaka 2022, kulingana na Benki ya dunia.
Kupanda kwa bei ya mafuta imechangia kupanda kwa bidhaa. Unga wa mahindi unaotumika kupika Ugali, chakula pendwa nchini, kimekua haba kwa wakenya wa kipato cha chini.
Nchi inashuhudia athari ya vita baina ya Urusi na Ukuraine- nchi mbili zinazochangia nafaka Kenya, ikiwemo ngano na mahindi.
Aidha, ukame uliokumbuka sehemu kubwa ya nchi umekua na athari mbaya kwa uzalishaji wa chakula cha mifugo, ambayo ni asilimia 22 ya pato la taifa linaloathirika na ongezeko la bei na uhaba wa mbolea, bidhaa maduhuli kutoka Ukuraine na Urusi. Wakati wa kampeni zake, William Ruto aliahidi ruzuku katika sekta hii ya uchumi wa Kenya.
Hali ya huzuni
Kikwazo kingine anachokumbana nacho Rais mpya ni ukosefu wa ajira ambapo asilimia 75 ya idadi ya watu wako chini ya miaka 35. Kila mwaka vyuo vikuu Kenya vinatoa takriban mahafali 500,000 katika soko la ajira, bila yoyote kujua vipi na wapi pa kuwaweka. Kulingana na takwimu za Benki ya dunia, kuna takriban watu millioni 5 waliokosa ajira - na katika sekta zisizo rasmi, mahali palipo na matumaini, kunatoa asilimia 80 pekee katika nafasi za ajira.
Kudhibiti ukosefu wa ajira, Rais Uhuru Kenyatta alitarajia ukuaji kupitia kuwekeza katika miundo msingi, ikiwemo kuwa na bandari ya kisasa Mombasa na ujenzi wa reli baina ya Nairobi na Mombasa. Kwa hali yoyote, sera hii imekuwa ghali na kuongeza deni la kitaifa mno - hususan kwa vile shilingi ya Kenya inazidi kudorora dhidi ya dola ya Marekani, kwa asilimia 5 kuanzia mwanzoni mwa mwaka, huku dola 1 ikiwa na thamani ya shilingi 120.45 kufikia september 13, 2022. Deni la kitaifa linakisiwa na Benki ya dunia kuwa dola milioni 70, ulipaji deni unagharimu asilimia 67 ya pato la kitaifa, na Uchina ikiongoza katika kudai Kenya.
Hii inatoa taswira kwamba kati ya mwaka 2013 na 2022, Nairobi inaongeza deni lake mara nne zaidi. Mary Goldman, mwakilishi wa Benki ya dunia, ana wasiwasi juu ya hatari ya ongezeko la deni na uendelezi wa ulipaji, huku akipatia wahusika tahadhari.
Wakati William Ruto ameahidi uwazi zaidi na udhibiti katika kuchukua madeni hususan kutoka Uchina, ufisadi ulokithiri ni donda sugu kwa jamii ya wafanyabiashara.
Ufisadi mkubwa na Rais mwenye utata
Katika takwimu za ufisadi mwaka 2021 zilizo chapishwa na shirika la Transparency International, kenya bado inavuta mkia, huku Nairobi ikiwa nambari 128 kati ya 180.
Rais mpya-- ambaye amejenga kampeni zake katika mikakati ya uchumi wa kijamii, huku akijitawaza kama “mkombozi tegemezi” -- itabidi sasa kuongoza kwa njia endelevu.
William Ruto anaandamwa na sifa za ufisadi. Katika ukosoaji Rais anayeondoka Uhuru Kenyatta kwa ghadhabu alimuita Ruto ‘mwizi’ katika kampeni. Kama kiongozi mwenye mali nyingi katika mifugo, kilimo, sekta ya ujenzi na hoteli, Rais mpya ana kazi ili kufaulu katika kumudu dhana na lawama za ufisadi na unyakuzi wa ardhi dhidi yake; ndio maana wapinzani wake wanamuita ‘mfalme wa kashfa’
Licha ya hayo, makamu wa Rais Rigathi Gachagua alitarajiwa kulipa fidia ya takriban dola milioni 1.7 kabla ya uchaguzi kwa kuhusika katika kesi ya ufisadi.
Ukame na dharura ya kibidamu
Hatimaye, Rais mpya atakabiliana na ukweli wa mabadiliko ya tabia-nchi. Sehemu za kaskazini na mashariki mwa Kenya wanakabiliwa na ukame hatari zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miaka 40. Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa, takriban watu milioni 2.5 wapo katika janga la uhaba wa chakula, ikiwemo zaidi ya watoto 460,000 chini ya umri wa miaka na takriban wanawake wenye ujauzito 90,000 wana utapiamlo.
Uchumi umesambaratika katika sehemu hizi kame Kenya ambapo wanategemea zaidi mifugo.
Takriban asilimia 50 ya mifugo iliangamia kwa ukosefu wa maji na lishe. Hata wanyama pori hawakusazwa: mizoga ya wanyama pori kama Twiga na Nyati imeshuhudiwa katika mbuga za wanyama. Jamii ya wafugaji wamelazimika kuuza mifugo ili kujikimu kimaisha.
Kwa mujibu wa Rais anayeondoka Uhuru Kenyatta, hali inayokubalika kuitwa “Janga la kitaifa” ililazimu Nairobi kuunda Mamlaka ya kitaifa ya kudhibiti ukame ambayo inasimamiwa kifedha na serikali na mashirika ya kimataifa. Hatahivyo mamlaka hii ina mapungufu makubwa ya fedha.
Hii inaonyesha kwamba hali ya kiuchumi na dharura za hali ya kibidamu ni changamoto zinazomkabili William Ruto; wakiwa na kibarua cha kupanda Mlima Kilimajaro, ulio na kilele cha juu zaidi Afrika, ambao unatizamia sehemu ya Kenya kwa shime.