Na Pauline Odhiambo
Katika biashara ya mitindo, unachokiamuru siyo kila wakati unachokipata, na linapokuja suala la mitindo ya Kiafrika, hakuna anayeweza kujaribu uvumilivu wako kama fundi cherehani.
Pale ambapo kucheleweshwa mara nyingi ni jambo la kawaida katika utoaji wa mavazi yaliyoshonwa kwa ajili yako maalum, mjasiriamali wa Kenya Beverlyn Mawia Muthengi aliona fursa ya kujaza pengo kwa kuunda mkusanyiko wa mavazi ya Kiafrika yaliyoko tayari ambayo yanafaa kwa tukio lolote, na hutolewa kwa wakati unaofaa.
Mavazi yake yamepamba nyota wa Hollywood kama Lupita Nyong’o na wanaharakati wengine maarufu ambao wamevaa mavazi yake yaliyotayarishwa kwa haraka.
“Niligundua kuwa watu wengi wana tatizo la kuaminiana linapokuja suala la kushughulika na mafundi cherehani. Yeyote aliye Nairobi anaweza kukuambia hadithi yao ya kuvunjwa moyo na mafundi. Hili ni tatizo kubwa katika nchi nyingi za Afrika,” Beverlyn anaambia TRT Afrika.
“Wakenya wengi pia ni wanunuzi wa dakika za mwisho. Tunaweza kujua kuhusu tukio miezi minne kabla lakini tutaanza kununua mavazi siku chache kabla ya tukio, ndiyo maana watu wengi huishia kuvunjwa moyo na mafundi cherehani,” anaongeza.
Wauzaji wengi mtandaoni duniani kote huahidi kutoa mavazi yaliyoshonwa vizuri lakini wanunuzi mara nyingi huishia kuvunjwa moyo mavazi yanapofika yakiwa yameonekana kama makosa ya ushonaji vya kile kilichoahidiwa.
Mitindo ya Kiafrika
Kabla ya kuanza biashara yake, Beverlyn alikuwa akihifadhi picha nyingi za mitindo yenye msukumo wa Kiafrika kwenye mtandao wa Pinterest, akihifadhi mitindo mengi mtandaoni alitafuta fundi cherehani wa kuaminika kutekeleza miundo hiyo.
“African Yuva ilianza kama biashara ya crotchet inayoitwa Yarn Yuva. Yuva inamaanisha ‘nyumbani’ kwa Kituruki na ‘nyuzi zilizosokotwa’ kwa Kihindi,” anaelezea. Wazo nyuma ya chapa hiyo lilikuwa kuunda lebo ya mavazi ya kimataifa inayowasilisha wazo la mitindo ya nyumbani iliyotengenezwa Afrika.
“Nilikuwa nje nikitafuta nyuzi siku moja nilipokutana na fundi huyu aliyekuwa akitengeneza mavazi na kitambaa cha Kiafrika. Nilimuomba kushirikiana nami na kunitengenezea sketi ndefu kutoka kwa kitambaa cha Kiafrika ili niweze kuziunganisha na crotchet nilizokuwa nikitengeneza. Hivyo ndivyo African Yuva ilivyoanzishwa mwaka 2017.”
Beverlyn alituma picha za mavazi yaliyomalizika kwenye mitandao yake ya kijamii na akaamka na wafuasi 8000 wiki chache baadaye.
“Hapo ndipo nilipogundua kuwa nilikuwa naelekea njia sahihi. Ukweli kwamba watu 8000 walihisi kulazimika kufuata ukurasa wangu ulithibitisha kuwa kulikuwa na mahitaji ya mitindo ya Kiafrika, na hiyo iliniwezesha kupanga biashara yangu vizuri,” anasema.
Alianza kuchora mavazi yaliyoongozwa na hisia zake za mitindo, akionesha mitindo yake ya kwanza mwaka 2018 licha ya bajeti ndogo. Rafiki wa Beverlyn alifananisha mavazi yote huku rafiki mwingine akichukua picha za kila vazi ili kutuma kwenye mitandao ya kijamii ya African Yuva.
Kwa mavazi aliyoshona mwaka 2019, Beverlyn alikuwa ameweka hela ya kutosha pembeni kuajiri mpiga picha na hata msanii wa mapambo kwa anuwai hiyo.
Anakumbuka kabati lake likivunjika mara mbili kutokana na uzito wa mikunjo mingi ya kitambaa cha Kiafrika iliyokuwa ikisubiri kubadilishwa kuwa miundo mizuri. Mkusanyiko uliomalizika ulikuwa hit ya papo hapo na uliona akipokea maagizo mengi ya mavazi yaliyotengenezwa kwa ajili ya mteja maalum.
Mavazi ya watu wenye miili mikubwa
“Mitindo yangu mwaka 2019 yalikuwa na vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mtindo maalum wa vazi ambao bado tunauza hadi leo. Tulipiga picha za mavazi yote yaliyotengenezwa ili wateja waweze kuona kwamba bidhaa inaweza kuwasilishwa kwao kama ilivyo, na sio kuwapotosha kwa matangazo ya uwongo kutumia picha za hisani kutoka kwenye mtandao kuuza kampuni,” anasema.
Mwaka 2019 nilivuta wimbi jipya la wateja kutoka Marekani na Ufaransa baadhi yao ni kampuni za mitindo zinazovutiwa na mavazi yaliyotayarishwa tayari.
“Jambo kubwa ambalo nalizingatia hadi leo kabla ya kutoa muundo wowote hutegemea kama unaweza kufaa wanawake wembamba na wanene,” anasema. “Hii pamoja na uthabiti wa ubora na utoaji wa huduma imeniwezesha kudumisha wateja wangu.”
Beverlyn amefanikiwa kutoa angalau mitindo mitatu kila mwaka tangu aanze biashara yake, lakini mwaka 2020, janga la Uviko-19 lilitishia kuvuruga rekodi yake.
Alihairisha kutoa dizain zake za kwanza wa mwaka 2020 hadi Aprili ilipobainika kuwa karantini iliwafanya watu wengi kugeukia majukwaa ya mtandaoni kwa ajili ya tiba ya rejareja.
“Nimefanya utafiti wangu na kugundua kuwa watu wengi walikuwa na nia ya kununua nguo za kuvaa kwa faraja wakati wa karantini, kwa hivyo nilitumia fursa hii kwa kubuni mavazi ya Kiafrika ya kuvaa nyumbani, barakoa na nguo nyingine zilizouzwa wakati huo,” anasema.
“Niliweza kuajiri mfanyakazi wangu wa kwanza mnamo Oktoba 2020. Nilihisi ni baraka kuweza kuajiri mtu wakati wa kipindi cha Uviko wakati watu wengi walipoteza ajira zao.”
Beverlyn sasa anajivunia kuwa na wafanyakazi 14 wakiwemo mafundi cherehani sita na meneja wa uzalishaji wanaotekeleza michoro na mawazo ya mitindo yake.
Inafaa hadi Hollywood
“Miundo yangu inaongozwa na hamu ya kuonekana mzuri na kujisikia vizuri wakati wote, na kwa hio lengo langu kuu ni kuunda chapa ambayo inaweza kuwapamba wanawake wote kwa uzuri kwa tukio lolote,” anaelezea.
Mwaka 2021, Lupita Nyong’o alivaa moja ya jumpsuits za Beverlyn wakati wa mahojiano kwenye kipindi maarufu cha televisheni kilichotangazwa Marekani. Mavazi mengine mengi ya Beverlyn yamevaliwa na waigizaji kwenye vipindi vya tamhtilia vilivyotangazwa na kampuni za utangazaji duniani kote.
“Awali nilitaka kubuni vazi la ajabu kwa Lupita lakini niliamua kuishia na muundo wa tayari ambao ulifanya kazi vizuri sana na mtindo wake. Uthibitisho tulioupata kama kampuni kutoka kwa nyota wa kimataifa aliyevaa moja ya mavazi yetu uliimarisha uwepo wetu kama chapa.”
“Chapa nyingi huunda kwa ajili ya wanawake kuangaliwa na wanaume, lakini kama African Yuva tunaunda kwa ajili ya macho ya kike,” anaambia TRT Afrika. “Yote ni juu ya kuunda chapa inayowaruhusu wanawake kuvutia na kusifu chaguo za mtindo wa kila mmoja huku ikiwajenga kila mmoja kupitia mitindo.”