Waziri wa Ulinzi wa Somalia Abdulkadir Mohamed Nur. Picha: Wizara ya Ulinzi 

Serikali ya Somalia imeendeleza vita vyake dhidi ya kundi la Al shabaab pamoja na kukabiliana na propaganda za kundi hilo ambalo limekuwa likitumia majina ya kiislamu kueneza ugaidi na kutekeleza mauaji dhidi ya watu wasiokuwa na hatia.

Wanajeshi wa Somalia wamekuwa kwenye mstari wa mbele katika vita dhidi ya Al Shabaab huku mbinu hii mpya ya majina ya vikosi hivyo ikionekana kusambaratisha fikra potofu ya Al shabaab.

Wizara ya ulinzi nchini humo, inaamini hatua hiyo itaimarisha vita vyake dhidi ya Al Shabaab ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiwapotosha watu kwa madai kuwa mapigano yake yalikuwa ni ya kidini na kuwaita walinzi wa Somalia watu wasiokuwa na dini au walioasi.

Hapo awali, vitengo mbalimbali vya wanajeshi wa Somalia vimekuwa vikiitwa majina tofauti kama vile Duufaan yaani Kimbunga, Gorgor au Tai, 14 Oktoba, na Haramacad kumaanisha 'duma'.

"Ali Bin Abi Taalib, Omar Binu Khadab na Khalid Bin Waleed ndio Waislamu rasmi na ni watu wema wanostahili kuigwa, na hivyo basi, tutachukua majina yao." Msemaji wa wizara ya ulinzi Jenerali Abdillahi Ali Aanod amesema.

TRT Afrika