Tiktok / Picha: Reuters

Wiki chache tu baada ya bunge la Kenya kupokea ombi la kuupiga marufuku mtandao wa TikTok nchini humo kutoka kwa baadhi ya walalamikaji, sasa rais wa nchi hiyo, William Ruto amevunj akimya chake juu ya mjadala huo na kusema kuwa kuna njia mbadala ya kufanya marekebisho juu ya utumiaji wa mtandao huo.

"Najua tumekuwa na mazungumzo kama taifa na kampuni ya Tiktok, na baadhi ya changamoto ambazo ziko katika mtandano huo.'' Ruto alisema.

Ruto anasema kuwa wamepanga kufanya mazungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa TikTok Shou Zi Chew kwa sababu Kenya inatoa kipaumbele kwa udhibiti wa maudhui na uchumaji wa mapato, kwa kuwa mifumo ya kidijitali huwawezesha waundaji maudhui kutanua talanta zao na kupata pesa.

"Kama nchi, kila mwezi tunapokea kati ya shilingi 300M hadi 500M kutoka kwenye majukwaa haya ya kidijitali, jambo ambalo linaongeza mapato yetu; tunahitaji kudhibiti athari hasi na badala yake kukuza zile chanya ambazo zinawafanya wasanii wetu, na waundaji wa maudhui kutanua talanta zao, kupata pesa, na kukuza vipaji vyao." Ruto alisema.

Kulingana na Ripoti ya hivi majuzi juu ya utumiaji ya mtandano kutoka Taasisi ya Reuters 2023, asilimia 54% ya watumiaji wa Intaneti nchini Kenya huchagua TikTok kama mtandao wa kijamii wanaoupenda kwa namna mbalimbali.

Tik Tok abayo imepata umaarufu mkubwa hasa miongoni mwa vijana imekumbwa na pingamizi katika siku za hivi karibuni kutoka kwa walalamikaji wanaodai kuwa imekuwa jukwaa na kusambaza dhana potofu zenye kuchafua maadili.

Marekani imetishia kufunga mtandao huo ambao unafuatiliwa na mamia ya mamilioni ya watu nchini humo huku Jimbo la Montana likiweka sheria mwezi Mei kupiga marufuku utumiaji wake.

Agosti 20 Serikali ya Somalia ilitangaza pia kufunga mtandao wa TikTok kufikia Agosti 24 ikitaja malalamiko hayo hayo y akupotosha maadili ya jamii.

Somalia imelalamikia pia kuwa mtandao huo umekuwa ukitumiw ana wanamgambo w aAl Shabaab kueneza itikadi zao na kusambaza picha za kutisha na mauaji.

TRT Afrika