Shajara ya safari: Fahamu Jiji la Yaounde

Ni jiji ambalo idadi yake ya watu hongezeka kila kuchao huku mamia ya watu wakiwasili kila siku kujaribu bahati yao ya kujipatia riziki. Ni jiji linaloendana sambamba na ndoto ya Afrika. Jiji la uwezekano mkubwa. Mwanahabari wetu wa TRT Francais anazuru Cameroon kukusogeza karibu na hali halisi ya taifa hilo; kaskazini mpaka kusini; magharibi hadi mashariki, kusudi upate taswira kamili ya Taifa la Cameroon. Leo ikiwa ndiyo siku ya kwanza ya safari yake; tayari amewasili Yaounde – ambao ni Mji Mkuu wa Cameroon.

Pindi tu mgeni anapowasili Yaounde, ni vigumu kuepuka kirutubisho cha klorofili; huku ukitupia jicho hali halisi ya harakati; kuanzia kwenye taswira ya vitongoji duni mpaka kwenye makazi ya kuvutia ya mabwenyenye wa Jiji, foleni ndefu za magari na misongamano ya watu huku kila mmoja akijishughulisha na harakati zake. Yaounde hukaribisha wageni wake na hisia fulani za ‘kijeuri hivi,’ watu tofauti kutoka maeneo tofauti na mandhari ya mji huu yanachangamsha kwa kweli.

Mji wa Yaounde upo katikati ya Cameroon huku hisia za msimu wa joto sampuli ya India zikikukaribisha. Rangi ya kijani si haba Yaounde. Hutosheki kuitazama. Kadhalika uzuri wa anga lake utakuvutia machoni.

Kasi na spidi ya madhari yake sio ya kuzoeleka kirahisi ila huna budi kukumbatia hali halisi hiyo. Kwa mbali kidogo huwezi ukapuuza hatari ya ufalme wa nyati. Msitu huu ambao zamani ulizingira kumbi za mikusanyiko sasa ishara ya uzalendo wa watu wa taifa la Cameroon. Yaounde ni mji ambapo nambari 7 ina uzito mkubwa. Ni mji wa milima 7. Makabila 7, wanawake 7 warembo, kumbi 7 na lugha 7.

Uzuri wa mandhari

Pembezoni mwa barabara ya leni nne ni miti ya kiasili iliyopambwa kwa madoido kama majenerali wa vikosi vya ulinzi. Mabango ya uchaguzi yangali yapo. Mara pindi tu unapopitiliza kupiga kona unakutana na bonde. Ishara ya usasa na ustaraabu inadidimia na kubaki uzuri wa migunga inayoshiba machoni.

Historia

Mnamo Novemba 30 mwaka 1889, mtaalamu wa mimea kutoka Ujerumani kwa jina Georg August Zenker alianzisha mji huo na kuupa jina Yaunde kwa heshima ya wakulima wa karanga wakati huo. Uzuri wa mjii huu hukuanza miezi michache iliyopita. Hapana. Ni mji ulio na historia kubwa. Kuanzia kwenye uwanja mkubwa wa michezo wa Olembe mpaka kwenye Wilaya ya Nkoldongo, eneo la makazi lililokarabatiwa kwa mtindo wa Marekani vilevile ni sehemu kubwa ya historia ya mji.

Yaounde imesimama juu ya machimbo yanayosadikiwa kuwa na udongo mzuri wa aina yake. Mji huu umeshuhudia wafanyakazi wa mataifa jirani ya Equatorial Guinea, Jamhuri ya Afrika ya Kati(CAR) na Guinea wakipita kwenda ughaibuni kufanya kazi.

Wanaofahamu vizuri mji huu tangu zamani wanakumbuka jengo la kwanza kutumika n Ujumbe maalum wa Serikali. Hilo ndilo lilikuwa jengo la kwanza kabisa kukarabatiwa Yaounde. Paa za jengo hilo zilikuwa kama vigae vya udongo na aliyeishi mahali hapo alikuwa ni Gavana raia wa Ujerumani kwa jina Hans Dominiki.

Kwa hakika vigae hivi vya udongo vinaeleza historia kubwa ya Mji huu kwa yeyote mgeni anayepita awe mwenyeji ama mtalii. Ni historia ambayo bila shaka ni ya aina yake na maalum kwa Yaounde.

TRT Français