Rais wa Pakistan Arif Alvi ametia saini agizo hilo baada ya Waziri Mkuu anayemaliza muda wake Sharif pamoja na kiongozi wa upinzani Raja Riaz kumchagua waziri mkuu wa kushikilia madaraka.
Taarifa fupi kutoka afisi ya rais wa Pakistani ilisema Alvi aliidhinisha jina la Kakar chini ya Kifungu cha 224A cha Katiba ya nchi.
Kakar anatokea jimbo la kusini magharibi la Baluhistan na ni mbunge huru, kulingana na tovuti ya Bunge la Pakistani.
Baada ya kula kiapo Jumatatu, Kakar atachagua Baraza lake la Mawaziri la muda kuendesha shughuli za kila siku hadi uchaguzi, unaotarajiwa kufanyika ndani ya miezi mitatu ijayo, uandaliwe.
TRT Afrika na mashirika ya habari