Chakula cha Ngalakh ni maarufu sana nchini Senegal wakati wa sherehe za Kikristo. Wakristo wamejenga mazoea ya kuwashirikisha kionjo hiki majirani zao Waislamu kama njia ya kuimairisha mahusiano.
Ngalakh ni mlo wa kitamaduni unaotayarishwa na familia za Kikristo za Senegali mwishoni mwa Kwaresima na kuwagawia majirani, jamaa, marafiki na wafanyakazi wenza wa Kiiislamu.
Ngalakh ni nini?
Ni aina ya uji mtamu ulioandaliwa kutoka mchanganyiko wa siagi ya karanga, unga wa ubuyu na unga wa mtama.
Wakati wa kupika uji wa mtama, wanachanganya na kimiminika cha siagi ya karanga, kisha wanatia matunda ya ubuyu. Hatua muhimu ni kukorogoa kwa muda mchanganyiko huo, kuchuja na kisha kuongeza ladha ya utamu. Wengine huongeza matunda yaliyokaushwa au chokoleti lakini wengine wanapendelea bila kuongeza chochote.
Marie De Souza tayari anajiandalia mlo wa mwaka huu. “Wengine tunajisikia vizuri kuwapa wenzetu Ngalakh. Ni njia ya kushirikisha sehemu ya baraka ya Pasaka na tunu zetu. "
"Ni utamaduni, lazima tuuendeleze hata kama ni ghali," anaendelea. “Kwa kuzingatia kiasi cha Ngalakh ambacho lazima familia zigawe siku ya Ijumaa Kuu, wengi huanza maandalizi siku moja kabla,'' anaeleza Marie De Souza.
Imani tofauti, tamaduni moja
Nchini Senegali ni jambo la kawaida kuona watu wa familia moja wakiwa wa madhehebu au imani tofauti kama Maimouna Diakhaté anavyotukumbusha.
“Waislamu wa Senegal wanaona kuwa wanawajibika kipekee katika kuandaa tamasha la Ngalakh. Jambo hili ni la kawaida kabisa kwa sababu katika familia nyingi za Wasenegal utakuta zina wazazi Wakristo na Waislamu. Ni jambo la kawaida sana kupata watu wa familia moja ambao si lazima washiriki dini moja,” aliiambia TRT Afrika.
Wengi wanasherehekea sikukuu hiyo wakiwa pamoja na marafiki au wanafamilia huku wakitakiana heri; na kufanyiana utani kuhusu sikukuu za kidini za imani zote mbili katika mitandao ya kijamii.
"Kwa miaka miwili, utani juu ya ubinamu kati ya Wakristo na Waislamu umechangiwa na uhamasishaji wa vijana kupitia mitandao ya kijamii. Wanaweka video na picha za vyakula huku wakifanyiana mizaha,'' anasema Maimouna Diakhaté.
Anahitimisha kwa kusisitiza umuhimu wa kuhifadhi mila hii ya kubadilishana chakula wakati wa sikukuu za kidini kwa kuwa "itachagiza na kuimarisha uhusiano wa kijamii kati ya Waislamu na Wakristo".