Nakafeero Josephine, 36, aliacha kazi yake ya zamani kama mtangazaji wa TV na kujiunga na tasnia ya mitindo kama mbunifu wa mitindo na mjasiriamali ambapo anamiliki chapa yake ya Jose House of Creations.
Akiwa na shahada ya biashara kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, pia alijiunga na NBS TV ya Uganda mwaka 2010 ambapo aliwasilisha maonyesho yanayohusu mitindo.
Uganda ikiwa ni nchi ambayo vijana wengi wanajihusisha na mitindo na kipindi chake kilifuatiliwa sana kwenye TV ambacho kilimsaidia kushinda tuzo mara mbili mwaka 2011 na 2012, Tuzo za African Walk.
Afrikan Fashion Walk Awards ni tamasha la kila mwaka la ubunifu wa mitindo ya Kiafrika ambapo lebo mpya na mitindo mapya huzinduliwa na kuonyeshwa pamoja na kuwazawadia na kuwatunuku waanzilishi, wakuu na washiriki wapya ambao wamejidhihirisha kwenye tasnia ya mitindo ya Kiafrika.
"Nilianza kazi za mitindo mwaka 2012. Ni zaidi ya miaka 9 nimekuwa kwenye Mitindo. Nilivutiwa na mavazi nilipokuwa nikionyesha vipindi vya TV pamoja na mastaa wa mitindo wa Uganda na kimataifa," anasema Josephine Nakafeero kwenye mahojiano pamoja na TRT Afrika.
Kupata vifaa vya kutengenezea nguo ni tatizo kwa wabunifu kama Josephine. Wengi wao wanalazimika kusubiri siku kumi ili mizigo waliyoagiza yafike katika ofisi zao.
"Tayari nimewavisha watu kadhaa wa Uganda na wa kigeni. Kwanza, tayari nimeshamtengenezea nguo aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Uganda. Vazi linalonipa sifa mjini ni ile niliyomvalisha mwimbaji na mwanasiasa maarufu Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine." asema Nakafeero.
Kwa watu wengi ambao wameishi Kampala, Uganda -Josephine, ni fahari kwao kwa sababu anatoa thamani kwa utamaduni wa Uganda duniani.
Uganda inajulikana kwa vazi la kitamaduni la "Gomesi" ambayo kulingana na wabunifu kadhaa wa mitindo wanasema kuwa Gomesi ndiyo inawapa heshima wanawake wa kiganda.
"Ninapenda ujasiri wa Bi Josephine kwa sababu alianzisha chapa yake ya kutengeneza Jose House of Creations kutoka dola 0 hadi hapa alipo. Tayari ameshatengeneza nguo za wanasiasa kadhaa," alisema Thomas Mbusa, mkazi wa zamani wa Jiji la Kampala, Uganda.
Kulingana na chama cha wazalishaji wa Uganda, Afrika Mashariki inatumia takriban dola za Marekani milioni 350 kununua nguo zinazoagizwa kutoka nje. Ukuaji ambao umeshuhudia mitindo ya Kiafrika ikipigania soko katika bara.
Kwa matamasha ya mitindo kama vile Kampala Fashion Awards, tuzo za mitindo Kampala katika mji mkuu wa Uganda, soko linatarajia kuvutia soko la nguo katika sehemu ya mashariki ya Afrika.
"Biashara yetu inahitaji ukakamavu, uvumilivu, kujitolea na ujasiri kwa sababu tunapaswa kufanya kazi muda wote. Ningependa kuudhihirishia ulimwengu kuwa nchini Uganda pia kuna mashabiki wa mitindo," asema Nakafeero.